Header AD

header ads

ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA WANAFUNZI NI MUHIMU KATIKA KUPUNGUZA AJALI



Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Kinondoni ACP Notker Kilewa amesema elimu ya Usalam Barabarani kwa Wanafunzi ni muhimu katika kupunguza ajali kwasababu Wanafunzi ni dhana muhimu ya kufikisha ujumbe na elimu ya usalama Barabarani kwa jamii nzima .

ACP Notker ameyasema hayo Wakati wa zoezi la utoaji wa Elimu ya usalama Barabarani kwa Wanafunzi wa shule ya Sekondari Oster ay Jijini Dar es Salaam liliratibwa na taasisi ya Tanzania Road Safety Initiative kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi leo Ijumaa Oktoba 21, 2022.


Notker amesema Wanafunzi wana uwezo wa kushika jambo kwa wepesi zaidi na ni waelezaji wazuri wa elimu.

Pia ametoa wito kwa madereva kuheshimu maeneo muhimu ya wanafunzi kuvukia barabara ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.


" Mfano tumewafundisha watoto namna ya kuvuka katika maeneo ya watembea kwa miguu hivyo tunategemea kwa madereva walikaa darasani kujifunza wataheshimu maeneo hayo kwasababu sheria zipo wazi " amesema Notka 

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Road Safety Initiative amesema kuwa wanampango wa kufungua klabu ya usalama barabarani kwa wanafunzi kwa lengo la kuwajengea uelewa wanafunzi kuhusu sheria za usalama barabarani na kuepuka ajali.


Baadhi ya wanafunzi waliopatiwa elimu ya usalama barabarani wameeleza kuwa watatumia elimu hiyo vizuri pindi wanapovuka barabara na watakua mabalozi wazuri kwa wenzao ambao hawakubahatika kupata elimu hiyo kuwaelekeza walochofundisha ili kuepuka ajali


ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA WANAFUNZI NI MUHIMU KATIKA KUPUNGUZA AJALI ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA WANAFUNZI NI MUHIMU KATIKA KUPUNGUZA AJALI Reviewed by Fahadi Msuya on October 21, 2022 Rating: 5