Tamasha la Kimataifa la Tanzanite latikisa jiji.
Na John Mapepele
Tamasha la pili la kimataifa la michezo kwa wanawake (Tanzanite) leo Oktoba 21, 2022 limeingia katika siku ya pili likipambwa na michezo mbalimbali iliyokuwa na hamasa kubwa kutokana na timu zote kujiandaa vizuri ukilinganisha na lile la kwanza.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 21, 2022 na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT) nchini Neema Msitha na kufafanua kuwa kiwango cha ubora wa michezo kimeboreshwa kutokana na mchujo uliofanyika wa kupata timu zinazoshiriki mwaka huu.
Kwa mujibu wa Msitha wachezaji wa Kabbadi wa timu iliyofuzu kucheza kombe la dunia Mwakani nchini India pia wameshiriki katika tamasha hili na kuleta mvuto wa aina yake.
Amesema matokeo kwa mchezo wa kabbadi, timu ya wanawake ya Buffalo imeiadhibu timu ya School Combine 52-20 huku katika mchezo wa mpira wa kikapu kwa wenye ulemavu timu ya wanawake ya Dar City imeibamiza timu ya Tembo 22-20.
Katika mchezo wa Karate Kata timu ya wanawake ya Tanzanite imeibuka kidedea dhidi ya Timu ya Coast kwa pointi 30-12 pia kwa upande wa karate Kumite, Tanzanite imeibamiza Coast 30-12.
Msitha amefafanua kuwa michezo itakayochezwa jioni hii ni baina ya Timu ya Netiboli ya Tanzania na Uganda na kumaliziwa na mapambano ya kukata na shoka ya ndondi ya kitaifa na kimataifa kabla ya kuhitimisha tamasha hili kesho kwa michezo mbalimbali.
Akifungua Tamasha hilo jana waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Mohamed Mchengerwa alielekeza BMT kusimamia kikamilifu michezo kuanzia wilayani ili kupata vipaji vingi vya wachezaji.
Tamasha la Kimataifa la Tanzanite latikisa jiji.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 21, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 21, 2022
Rating:




Post a Comment