Header AD

header ads

MHE. MCHENGERWA AWATAKA WATANZANIA KUTUMIA BIMA KUTOKA NIC.



Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Watanzania kutumia huduma za Bima kutoka NIC kwa kuwa zinakidhi ubora na kujibu changamoto za Wananchi.

Akizungumza hayo kwenye kwenye hafla ya kuikaribisha nyumbani na kuipongeza timu hiyo kwa kufika robo fainali kwenye mashindano ya kombe la Dunia 2022 yaliyofanyika nchini Uturuki.

“Natamani kuona wananchi wanafahamu na wanatumia Huduma za Bima kutoka NIC kwani zina ubora na ni Shirika la Watanzania wenyewe” alisema  Mchengerwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Dkt. Elirehema Doriye amesema kuwa NIC imetoa kiasi cha shilingi Mil. 40 kama pongezi kwa timu ya Taifa ya walemavu Tembo Warriors kwa kufikia hatua ya robo fainali katika mashindano hayo.


”Kwa kutambua umuhimu wa Tembo Warriors na shughuli mliyokwenda kuifanya kwenye kombe la Dunia NIC tumetoa Mil. 40 kama pongezi kwa timu kwa kufika robo fainali na isiwe mwisho wa nyinyi kukata tamaa”, alisema Dkt.  Doriye.

Aidha Dkt. Doriye ameipongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo chini ya Waziri Mchengerwa kwa kazi nzuri ya kukuza na  kuendeleza michezo nchini .
MHE. MCHENGERWA AWATAKA WATANZANIA KUTUMIA BIMA KUTOKA NIC. MHE. MCHENGERWA AWATAKA WATANZANIA KUTUMIA BIMA KUTOKA NIC. Reviewed by Fahadi Msuya on October 11, 2022 Rating: 5