Header AD

header ads

NHC YAKABIDHI VIFAA VYA UJENZI VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 2.5 MKOANI MARA



SHIRIKA la Nyumba la Taifa NHC lime kabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi ikiwemo saruji mifuko 91, nondo 26 na kilo moja ya misumari  vikiwa na thamani ya Shilingi Mil. 2.5 kwa ajili ya kuchangia  ujenzi wa vyumba viwili   vya madarasa katika shule ya  Sekondari Busegwe  inayojengwa katika  Wilayani ya Butiama Mkoani Mara. 

Msaada huo umekabidhiwa Oktoba 3, 2022 eneo hilo la ujenzi wa Shule hiyo katika kata ya Busegwe  na Meneja wa NHC Mkoa wa Mara Eliaisa Keenja  kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Nehemia Kyando. 



Keenja amesema, wametoa msaada huo kufuatia maombi yaliyotolewa na Wadau wa maendeleo kutoka kata hiyo walioomba  wasaidiwe ujenzi wa jengo hilo linalojengwa kwa michango ya wadau. Kufuatia maboma mawili  kukamilika kutokana na michango na  nguvu  kazi za  wananchi.  


Msaada huo unalenga kukamilisha boma hilo,  ili Serikali  ikamilishe hatua ya kuezeka  kusudi yawasaidie wanafunzi wa kata hiyo wanaotembea  kwenda kusoma katika Shule ya Sekondari Butuguri umbali mrefu wa Km 14. 

"Shirika la NHC  limekuwa likisaidia kuunga mkono juhudi mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na serikali  kwa jamii. Na ndio maana tumekabidhi vifaa hivi visaidie ujenzi wa jengo hili ambalo linajengwa kwa nguvu za wadau wa maendeleo nasi tukiwa sehemu ya wadau wa maendeleo tumeona tutoe msaada huu usaidie Watoto ambao wanatembea umbali mrefu  kama tulivyoambiwa wasome karibu na kwao." amesema Keenja. 


Mwenyekiti wa Wadau wa  ndani  wa maendeleo  Richard Mkoji amesema zamani ilikuwa kata moja ya  Butuguri  baada ya kutengwa wakaona ni vyema waanzishe shule hiyo wawasaidie watoto wao adha ya kutembea   umbali wa  km 14 kwenda Butuguri kusoma. 

"Tuliwaomba NHC watusaidie kukamilisha boma letu walau watupe saruji na nondo, bahati nzuri wametupatia msaada huo  tunashukuru sana kwa msaada wao  na niombe wadau mbalimbali watusaidie kujenga shule hii ambayo itakuwa mwarobaini kwa watoto wetu kutembea umbali mrefu na kuepukana na vishawishi njiani  kutoka kwa madereva boda boda." amesema Mkoji.

"Kata yetu ya Busegwe ina vijiji vitatu ambavyo ni nyanza, Busegwe na Kigori ujenzi huu unafanywa kwa nguvu za wananchi kujitolea kwa kushirikiana na Wadau ulianza mwaka jana matarajio yetu yakienda  vizuri naamini serikali itamalizia hatua ya mwisho ya kukamilisha ili kusudi shule ianze maana pia ujenzi wa nyumba ya Mwalimu unaendelea kwa nguvu za wananchi."amesema Mkoji.


Ibrahimu Bukume ni Katibu Mwenezi wa Chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Busegwe amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kuunga mkono utekelezaji wa ilani ya Chama Cha mapinduzi Kupitia msaada huo. 

"Chama cha mapinduzi kinefurahi kwa hatua hii muhimu ambayo NHC wamefanza Kama wadau wa Maendeleo kuunga juhudi za serikali inayoongozwa na CCM naamini kabisa msaada wao utakamilisha boma na pia niombe wadau wajotokeze kushiriki shughuli hii na kuchangia Maendeleo mbalimbali." amesema Bukume. 

Neema Japheti ni Mkazi wa Busegwe (54) ambapo amesema wanafunzi wamekuwa wakitembea umbali mrefu kwenda shule na kwamba Watoto wa kike wamekuwa wakipata vishawishi wakiwa njiani kutoka kwa waendesha boda boda  na pia kufika wakiwa wamechoka shuleni hali ambayo inaathiri maendeleo yao kitaaluma.
NHC YAKABIDHI VIFAA VYA UJENZI VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 2.5 MKOANI MARA NHC YAKABIDHI VIFAA VYA UJENZI VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 2.5 MKOANI MARA Reviewed by Fahadi Msuya on October 04, 2022 Rating: 5