WAANDISHI WA HABARI WAPEWA MAFUNZO YA UELEWA WA MAGONJWA YA AFYA YA AKILI
Katika kutambua mchango wa vyombo vya habari kuelimisha jamii kutunza afya ya akili, Wizara ya Afya kupitia kitengo cha afya ya akili imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuelewa kuhusu afya ya akili.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika Jijini Dar es salaam Mratibu wa Afya ya akili Halmashauri ya Kinindoni Dkt. Mwendo Peter amesema kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kufikia idadi kubwa ya wanajamii na kuwapa elimu sahihi ya kuwawezesha kutunza afya ya akili.
Akizungumzia kuhusu kumtambua mtu mwenye ugonjwa wa akili dalili moja wapo ni kwamba mtu anakua yupo tofauti na watu wengine huku kwa upande wa mtoto anakua mtundu sana pia anakua amevuka hatua ya sita na anaweza kufanya vitu tofauti na watoto wengine.
"Unakuta mtoto anaonesha baadhi ya dalili mfano kujitenga, kupigapiga wenzake, na wengine husema kuna watu wanawakimbiza watu ambao kiuhalisia hawapo, amesema Dkt. Mwendo"
Mafunzo hayo ya uelewa wa afya ya akili kwa waandishi wa habari ni muendelezo wa kuadhimisha wiki ya afya ya akili duniani ambayo ilizinduliwa Oktoba tatu katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni " Afya ya akili ni kipaumbele kwa wote"
WAANDISHI WA HABARI WAPEWA MAFUNZO YA UELEWA WA MAGONJWA YA AFYA YA AKILI
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 05, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 05, 2022
Rating:

Post a Comment