Header AD

header ads

SERIKALI YAWASILISHA MPANGO KABAMBE WA KITAIFA WA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA KWA WADAU WA MAENDELEO



Katibu Mkuu Ofisi ya Makmu wa Rais Bi. Mary Maganga akifungua kikao cha Ofisi ya Makamu wa Rais na Washirika wa Maendeleo kilichofanyika leo Oktoba 13, 2022 katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaban akizungumza wakati wa kikao Ofisi ya Makamu wa Rais na Washirika wa Maendeleo kilichofanyika leo Oktoba 13, 2022 katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.



Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Kundi la washirika wa Maendeleo nchini (Development Partners Group on Environment, DPG) Bw. Zlatan Milisic akizungumza wakati wa kikao Ofisi ya Makamu wa Rais na Washirika wa Maendeleo kilichofanyika leo Oktoba 13, 2022 katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Thomas Bwana akiwasilisha Mpango Kabambe wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira wa mwaka 2022-2032 wakati wa kikao na Washirika wa Maendeleo.


Katibu Mkuu Ofisi ya Makmu wa Rais Bi. Mary Maganga (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine na Washirika wa Maendeleo baada ya kufungua kikao kilichofanyika leo Oktoba 13, 2022 katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.


Na Yusuph Digossi- Dar es Salaam


Katika kuhakikisha uratibu wa mazingira unafanyikia vizuri, kitaalamu na ufasaha Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa mpango kabambe utakaotekelezwa kwa miaka 10 kwa lengo la kubainisha changamoto za Kimazingira zinazopatikana nchi nzima na kuweka mapendekezo ya kutunza mazingira na uoto wa asili.

Baada ya kuandaliwa kwa mpango kabambe huo leo Alhamisi Oktoba 13, 2022 Ofisi ya Makamu wa Rais imekutana na wadau wa maendeleo upande wa mazingira kwa lengo la kuwaonyesha kilichofanyiwa kazi katika mpango kabambe huo .

Akizungumza wakati akifungua kikao hicho Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Marry Maganga amesema kuwa kupitia kikao hicho wadau hao wataangalia maeneo ambayo mpango kabambe umeyaainisha na kutoa mapendekezo ili kushirikiana kwa pamoja kutatua changamoto zilizopo.

" Kwenye mpango kabambe huu tumeonyesha maeneo mbalimbali yenye changamoto za Kimazingira ikiwemo ufugaji ambao haufati taratibu nakuharibu ardhi, maeneo yenye ukame, maeneo ya pwani yaliyoharibiwa mikoko, na changamoto nyingine za Kimazingira hapa nchini " amesema Marry Maganga

Ameongeza kuwa lengo la mpango huo si tu kuanisha changamoto lakini pia kuweka mapendekezo ya namna ya kurudisha nchi ya Tanzania katika hali yake ya asili.

Kwa upande wake  Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Thomas Bwana  amesema kuwa matarajio yao baada ya kikao hicho wadau wote watashirikiana na kila mmoja atachukua hatua yake ili kuboresha mazingira.
SERIKALI YAWASILISHA MPANGO KABAMBE WA KITAIFA WA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA KWA WADAU WA MAENDELEO SERIKALI YAWASILISHA MPANGO KABAMBE WA KITAIFA WA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA KWA WADAU WA MAENDELEO Reviewed by Fahadi Msuya on October 13, 2022 Rating: 5