HAKUNA KIJIJI KITASAJILIWA BILA KUSHIRIKISHA WIZARA ZA KISEKTA- David Silinde
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.David Silinde (Mb) amesema Serikali imeiagiza Mikoa na Wilaya kutosajili kijiji au maeneo mapya ya utawala bila kushirikiana na Wizara nyingine za kisekta.
Mhe. Silinde ameyasema hayo Oktoba 12, 2022 mkoani Katavi wakati wa ziara ya Mawaziri wa Kisekta ya kutatua migogoro ya ardhi katika vijiji 975.
"Hatutasajili hayo maeneo mpaka kuwepo na ushauri au mapendekezo kutoka kwa Wizara za Kisekta kama Maliasili, Ardhi na nyinginezo," amesisitiza Mhe. Silinde.
Amesema hatua hiyo ya Serikali imelenga kuondokana na changamoto za migogoro ya ardhi zinazoendelea kujitokeza nchini.
Ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta itaendelea katika Mkoa wa Geita.
HAKUNA KIJIJI KITASAJILIWA BILA KUSHIRIKISHA WIZARA ZA KISEKTA- David Silinde
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 14, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 14, 2022
Rating:

Post a Comment