Header AD

header ads

SHAKA AZINDUA MSIMU WA KILIMO MOROGORO.



Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amezindua msimu wa kilimo katika Mkoa wa Morogoro na kuwataka wananchi kutumia vyema fursa mbalimbali zinazotengezwa na serikali ili kujiletea maendeleo.

Uzinduzi huo ameufanya leo katika Kituo Cha Utafiti wa Kilimo (TARI) Ilonga, kilichopo wilayani Kilosa Mkoa wa Morogoro ambapo amesema miongoni mwa fursa hizo ni pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na kuanza kufanya kazi kwa treni ya mwendo wa haraka.

Pia, Shaka amesema uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuyatwaa na Kuwapa Wananchi  mashamba 11 yaliyokuwa mikononi mwa wawekezaji ambao kwa muda mrefu wameshindwa kuyaendeleza, ni moja ya mambo makubwa ya kupigiwa mfano na kupongezwa yaliyofanywa na Rais Samia.



SHAKA AZINDUA MSIMU WA KILIMO MOROGORO. SHAKA AZINDUA MSIMU WA KILIMO MOROGORO. Reviewed by Fahadi Msuya on October 04, 2022 Rating: 5