WADAU WA AFYA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI
Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuboresha huduma za afya nchini nchini , Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia idara ya afya imesema kuwa itahakikisha kwamba inaboresha matumizi ya Takwimu kwenye utoaji wa huduma bora za afya katika vituo vya kutolea huduma
Hayo yamesemwa na Mratibu wa huduma za ubora kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Idara ya Afya Dkt. Pius Kagoma wakati akishiriki Mkutano wa sehemu ya maandalizi ya Kongamano la kila mwaka la Afya(Tanzania Health Summit) litakalo waleta pamoja serikali, sekta binafsi na wafanyabiashara kuanzia wiki ijayo(Oktoba 11 hadi 13) jijini Dar es Salaam.
Mratibu huyo amesema kuwa Rais Samia alitolea msisitizo suala la uboreshaji wa huduma za afya hivyo Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya watahakikisha wanamuunga Mkono Rais Samia kwa kuhakikisha wanaboresha eneo hilo.
“Serikali kwa miaka 10 imekuwa ikijikita katika ujenzi wa miundombini na kuimarisha watumishi wa afya sasa kama mtakuwa mkumbuka wakati Rais anatine saini kwenye mkataba wa lishe alizungumza uboreshaji wa huduma za afya sisi tunamuunga mkono" amesema
Kwa upande wake Rais wa THS Dk Omary cheyo,asema watazungumzia kuhusu mifumo ya bima ya afya,mifumo ya uendeshaji wa madaraka katika sekta ya afya ,utafiti na uvumbuzi na mambo mengi ambayo yanahusiana na magonjwa.
“Mkutano huu tunapanga kujadili utoaji wa huduma bora za afya tumeona changamoto kubwa katika nchi ubora wa afya bado unasuasua wadau watakutana kwa kina kwa kiasi gani tumejifunza,tuko wapi,tufanye mikakati gani kutokana na uzoefu wa jumla ili kutatua tatatizo,”amesema
WADAU WA AFYA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 06, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 06, 2022
Rating:



Post a Comment