Header AD

header ads

WADAU WA HAKI ZA WANAWAKE WAANDAA NDAA JUKWA LA MSICHANA " GIRL'S AGENDA FORUM 2022"



Katika kusherekea siku ya mtoto wa kike dunuiani yenye kauli mbiu " wakati ni sasa haki zetu kesho yete" ambayo huadhimishwa Oktoba 10 kila mwaka ambayo inalenga kutambua na kusherehekea mafanikio ya wasichana na kuangalia changamoto zinazowakumba watoto wa kike mashirika ya Sema Tanzania, Falaviana Matata Foundation, Girls effect , Msichana Iniative na Tai Tanzania yataendesha Ajenda ya jukwaa la msichana " Girls Agenda Forum 2022" 

Akizungumza na waandishi wa habari  mwakilishi wa taasisi hizo  amesema kuwa jukwaa hilo limelenga kuwaleta pamoja wasichana kutoka maeneo mbalimbali na wadau wa haki za wasichana ili kusherehekea mafanikio ya wasichana na kuleta kwa pamoja changamotyo mbalimbali zinazowakabili wasichana.


Kuhusu shughuli walizofanya kabla ya Ajenda ya wasichana amebainisha kuwa walifanya kazi mbalimbali katika maeneo ya Dododma, Tabora, Iringa , Lindi Shinyanga na Visiwani Zanzibar ili kufiki wasichana wenzao na jamii na kutoa elimu kuhusu changamoto zinazowakabili wasichana.

"Shughuli hizi tuliweza kufanya kupitia Midahalo, Mabonanza, Ngoma , Michezo, Nyimbo, maigizo na shuguli nyinginezo"  amesema 


Ameongeza kuwa kupitia shughuli hizo waliweza kufikia Wasichana 2103 kutoka Mikoa tajwa hapo juu ambapo ziliangalia kuhusu sheria na sera zinazokwamisha wasichana kupata elimu haswa sheria kandamizi ikiwemo sheria ya ndoa ya mwaka 1971.

Kwa upande wake Neema Nickson, mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Shaban Robert ametoa wito kwa wadau wa haki za wasichana kuendelea kutoa elimu katika jamii kuhusu madhara ya ndoa za utotoni ili watoto wa kike wasionekane kama chanzo cha kipato na kuozwa mapema na wapate haki ya elimu kama ilivyo kwa watoto wa kiume.


Amesema Serikali itoe adhabu kali kwa watu wanaooa na kuhusika katika kuozesha wasichana wenye umri mdogo ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo ili kutokomeza viotendo hivo katika jamii.
WADAU WA HAKI ZA WANAWAKE WAANDAA NDAA JUKWA LA MSICHANA " GIRL'S AGENDA FORUM 2022" WADAU WA HAKI ZA WANAWAKE WAANDAA NDAA JUKWA LA MSICHANA " GIRL'S AGENDA FORUM 2022" Reviewed by Fahadi Msuya on October 11, 2022 Rating: 5