WALIOCHUKUA MAHARI KWAAJILI YA KUWAOZA WATOTO WATAKIWA KUZIRUDISHA
Waliochukua fedha ya mahari kwaajili ya kuwaoza wasichana waluomaliza darasa la Saba mwaka huu warudishe haraka.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere mkoani Pwani Omary Pumzi wakati akihutubia kwenye mahafari ya shule ya msingi Muungano huko kwa kwa mfipa Kibaha mkoani Pwani.
Omary amesema Kuna Wazazi wanatabia ya kutojali haki ya kumpa elimu mtoto wa kike na inawezekana tayari wameshachukua fedha za wanaume kwaajili ya kuwaoza Wahitimu wa darasa la Saba mwaka huu warudishe haraka kabla hatua za kisheria hazijafuata mkondo wake.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Faith Thawe alisema kuwa changamoto kubwa ni shule hiyo kukosa uzio hali inayosababisha wizi wa mali za shule.
Ameyasema hayo wakati akizungumzia na Waandishi wa Habari kwenye Mahafari ya shule ya msingi Muungano huko kwa kwa mfipa Kibaha mkoani Pwani.
Kwa upande wake Mariam Mbinda akisoma risala ya wahitimu alisema kuwa upungufu wa vyoo 33 vya wanafunzi ni changamoto kubwa sana kwani yaliyopo ni nane tu wanafunzi 79 walitunukiwa vyeti vya kuhitimu masomo ya elimu ya Msingi.
WALIOCHUKUA MAHARI KWAAJILI YA KUWAOZA WATOTO WATAKIWA KUZIRUDISHA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 24, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 24, 2022
Rating:



Post a Comment