WATAKIWA KUONDOKA KWENYE ENEO WANALOISHI KWA ZAIDI YA MIAKA 40
Na Hadija Bagasha Tanga.
ZAIDI wakazi 7000 wa eneo la Bondo kata ya Kwamagome Wilayani Handeni Mkoani Tanga wamekumbwa na taharuki baada kutakiwa kuondoka kwenye eneo wanaloishi kwa zaidi ya miaka 40 na kuhamia kusikojulikana kupisha eneo hilo ambalo linadaiwa ni mali ya Wakala wa huduma ya Misitu Tanzania TFS jambo ambalo wamemuomba Rais Samia, Suluhu Hasan kuingilia kati mgogoro huo.
Watu zaidi ya 7000 wamekumbwa na hofu ya kuondoka kwenye eneo hilo wanaloishi na kuhamia kusiko julikana.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye eneo hilo wakiwa na viongozi mbalimbali serikali na chama wananchi hao wamesema wanasikitika kuondolewa kwenye eneo hilo huku wakiwa hawajui wapi watakapokwenda.
Wananchi hao wamesema kilio chao ni kwa Rais Samia Suluhu Hassan dhini ya muda wa miezi miwili waliopewa kuondoka kwenye eneo hilo na hawajui ni wapi watakwenda huku eneo hilo likidaiwa ni la hifadhi.
Wananchi hao wamedai eneo hilo wameishi toka enzi za mababu zao wakilitumia kwa ajili ya kilimo na mifugo na kuhamishwa kwa namna hiyo wanasema waataathirika kiuchumi.
Akizungumza na kituo hiki mmoja wa wananchi hao amesema kuwa hawajui ni wapi watakapokwenda hivyo kilio chao ni kwa Rais wao mpendwa Samia Suluhu Hassan wakidai haki zao zinapotezwa kwani wanaondolewa bila kuambiwa wanapelekwa wapi.
"Mheshimiwa tuende wapi leo tukalime wapi na maisha yalivyokuwa magumu ninakuomba kwa uweza wa Mungu muambie mama ageuze uso wake aangalie Bondo aangalie familia zetu zitakwenda wapi, "alisisitiza Mmoja wa wananchi hao.
Diwani wa eneo hilo Mussa Mkombati anaililia serikali dhidi ya agizo la kuhama wananchi hao kwene hilo ambalo wananchi wanalitumia kupambana na maisha yao huku Mbunge wa jimbo hilo Ruben Kwagilwa anasema serikali inatakiwa kutizama upya agizo hilo kwa maslahi ya wananchi wake.
"Kwa heshima na taadhima mheshimiwa Rais napiga goti hili nikikuomba unisaidie kuwaokoa wananchi hawa ambao mpaka sasa hawajui wapi watakwenda sina pakkuupeleka umati huu unaouona mbele yangu, "alisema Mkombati.
Mbunge wa jimbo hili Ruben Kwagilwa anasema serikali inatakiwa kutizama upya agizo hilo kwa maslahi ya wananchi wake.
"Watendaji wetu ndani ya serikali wasitake kumchonganisha mheshimiwa Rais na wananchi hawa tunamuomba mheshimiwa Rais wananchi hawa Bondo waendelee na maisha yao hapa Bondo, "alisema Mbunge Kwagilwa.
Hivi karibuni kamishna wa wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS Prof Dos santos Silayo akiwa Mkoani Kilimanjaro alisisitiza msimamo wa serikali juu ya wananchi waliohamia maeneo ya hifadhi mnalimbali za misitu hapa Nchini.
"Hifadhi zetu za misitu hifadhi za wanyapori zimetengwa kwajili ya manufaa mapana ya Taifa letu katika maeneo haya yaliyohifadhiwa hayaruhusiwi kuingia na kufanya shughuli ambazo sio rasmi hivyo katika maeneo yote ambayo wanachi wametwalia kwa mamlaka ya kuingia na kufanya shughuli katika misitu hiyo kama ambavyo imeshatamkwa mara kadhaa na viongozi wetu wakuu wa nchi wanapaswa kuondoka kwenye maeneo hayo, "alisisitiza Prof Silayo.
Kitendawili ni wapi wananchi hawa watakwenda mara baada ya kuhama kwa lazima, huku shule ya msingi iliyopo katika eneo hilo ikiwa na wanafunzi 700 ambao nao ni kitendawili watahamishiwa shule gani baada ya hapo .
WATAKIWA KUONDOKA KWENYE ENEO WANALOISHI KWA ZAIDI YA MIAKA 40
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 18, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 18, 2022
Rating:






Post a Comment