Header AD

header ads

WAZIRI KAIRUKI ATEMBELEA WAKALA WA MABASI YAENDAYO HARAKA - DART





OR TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah J. Kairuki akiwasili Makao Makuu ya Ofisi za Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Dar es salaam na kupokelewa na Mkurugenzi wa DART, Dkt. Edwin Mhede. Leo tarehe 10 Oktoba 2022


Waziri Kairuki atafanya ziara ya siku mbili katika Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ambapo siku ya kwanza atapokea Taarifa ya utendaji wa DART na kuongea na Menejimenti ya Wakala pamoja na Watumishi wa DART.

Siku ya pili, atatembelea  Miradi ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa kukagua vituo vya mabasi na huduma zinazotolewa kuanzia kituo cha Mabasi cha Kimara mpaka Mbagala.



WAZIRI KAIRUKI ATEMBELEA WAKALA WA MABASI YAENDAYO HARAKA - DART WAZIRI KAIRUKI ATEMBELEA WAKALA WA MABASI YAENDAYO HARAKA - DART Reviewed by Fahadi Msuya on October 10, 2022 Rating: 5