WAZIRI NAPE AZINDUA MFUMO MPYA WA POSTA KIGANJANI.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) akitembelea banda la maonesho la Shirika la Posta wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani tarehe 9 Oktoba 2022, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, (Kulia) ni Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta, Macrice Mbodo ( Kushoto) ni Katibu Mkuu wa Wizara wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrise Mbodo akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Posta duniani katika ukumbi wa Julius Nyerere Internationa Convention Centre, jijini Dar es Salaam Oktoba 09, 2022.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akifurahi jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani tarehe 9 Oktoba, 2022, katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC).
Mkurugenzi wa biashara kutoka lipa kwa uhakika, Kelvin Mayala akimapatia maelezo Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye mara baada ya kutembelea banda lao wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani tarehe 9 Oktoba, 2022, katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC).
Mkurugenzi wa biashara kutoka lipa kwa uhakika, Kelvin Mayala akimapatia maelezo Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye mara baada ya kutembelea banda lao wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani tarehe 9 Oktoba, 2022, katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC).
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye amezindua Stampu ya Pamoja yenye historia ya Tanzania na nchi ya Oman, wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani tarehe 9 Oktoba mwaka 2022 yenye Kauli Mbiu ya Posta kwa kila mtu.
Sambamba na hilo Waziri Nape amezindua mfumo mpya wa Posta Kiganjani ambao utabeba huduma zote za shirika la Posta na kuziweka mahali pamoja ndani ya simu ya kiganjani.
Akizungumza wakati Uzinduzi huo uliofanyillka Leo jijin dar es Salaam Waziri Nape amesema Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Samia imejipanga kuwawazesha watoa Huduma za posta kuwafikia wananchi Kwa urasi bila kufika Katika ofisi za posta.
"Hili litawezekana kwakuwa Serikali imekalisha utekelezaji wa mfumo wa Anuani za Makazi ambao ni miundombinu Muhimu Katika utoaji wa Huduma" amesema Waziri Nape.
Pamoja na Hayo Waziri Nape amesema historia ya Oman na Tanzania ni ndefu na imezunguka sana ni muhimu historia hii ikalidwa na wao shirika la posta wameamua kulinda historia hiyo.
Pia waziri amewapongeza viongozi wa shirika la Posta wa Tanzania na Oman Katika kushirikiana na kuzindua stempu ya Pamoja.
Hata hivyo Waziri ameto wito Kwa shirika la Posta kuongeza Nguvu Kwenye kubuni biashara nyingine za kiposta zinazoenda na matuzi ya Technolojia Ili kukithi mahitaji mapya ya wateja.
Aidha Waziri Nape amemkabidhi Mshindi wa Uandishi wa Makala, Bi. Jacqueline J. Liana mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Posta.
"Waziri Nape amewasihi wa Watanzania kutumia Huduma za posta ambazo zimeboreshwa kwakuwa posta ya Sasa si barua tuuh ni Zaid ya barua" amesema Waziri Nape.
WAZIRI NAPE AZINDUA MFUMO MPYA WA POSTA KIGANJANI.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 09, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 09, 2022
Rating:





Post a Comment