ZOEZI LA KUPIGA KURA TUZO ZA " CONSUMER CHOICE AWARDS" LAZINDULIWA RASMI
Na Mwandishi wetu
Zoezi la upigaji kura katika tuzo za chaguo la mteja Afrika (Consumer Choice Awards Africa) limezinduliwa rasmi ambalo litaanza oktoba 9, 2022 na litaendelea kwa mwezi mmoja hadi tarehe 2 Novemba 2022.
Hayo aliyasema, Mkurugenzi wa Lavine International Agency Limited, Diana Laizer wakati wa uzinduzi huo na kusema kuwa tukio la utoaji tuzo za biashara ni linatambua, linaboresha na kukuza ubora wa biashara kupitia chaguo la watumiaji.
"Kuna vipengele ambavyo vinahusisha makampuni na wafanyabiashara ambao siyo watanzania, ambao vinagusa ukanda wa Afrika Mashariki, Afrika Magharibi na Afrika Kusini, tumeweza kufanya hivyo kwa mwaka wa kwanza na huu ni mwaka wa pili"
Laizer alisema ipo kampuni mpya ambayo inathibitisha na usiku wa upigaji kura mshirika kutoka Audiax International.
Pia Laizer alisema washiriki wa Tuzo hizo za chaguo la mteja Afrika 2022 wanatangazwa kupitia mitandao ya kijamii na gazeti la mwananchi.
Kwa upande wake, Meneja huduma za jamii kutoka Benki ya Absa Tanzania, Hellen Siriya alisema benki yao wanatambua kwamba Consumer Choice Awards inaendana na mwenendo wao kama Benki ya kwamba unamuweka mteja katikati ya kile kitu unachokifanya au kukipanga.
"Consumer kwetu sisi ni mdau, ni mteja na ni yule mtu anayeamini Brand yako, hivyo ni kitu ambacho kilitupa kipaumbele sana kuona kwamba ni kitu ambacho tunaweza kukifanya kushiriki siyo tu kudhamini lakini pia kutambua mchango wa wale consumers na wadau na makampuni mengine yote ambayo inatoa ile nafasi katika kushiriki na kutambua mchango wa wale ambao wanaamini brand yako"
Siri ya alisema Bank ya Absa ni sehemu ya kutoa kwenye jamii kwamba wanaangalia huduma za jamii ambazo zinagusa kila nyanja ikiwa ni kwenye Elimu, ujasiriamali, Afya n.k
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Auditaxe International, Straton Makundi alisema wanayo furaha kushiriki katika zoezi hilo la kuhakikisha zoezi zima la kupiga kura linakwenda sawa sawa na kila kura inayopigwa inahesabiwa.
"Tutakua tunahakikisha hakuna anayeingilia mfumo wa upigaji wa kura hivyo matokeo yatakapotoka, mshindi atapatikana kwa halali"
Makundi alisema consumers wataweza kupiga kura kwenye website ya consumer choice awards Afrika na vipengele vyote 74 utazikuta.
"Ili uweze kupiga kura Utatakiwa kujisajili kwa kuingiza Email yako na utakapopata link itakupeleka kwenye hivyo vipengele na utaweza kuchagua kipengele unachokitaka wewe na utatakiwa kupiga kura mara moja tu kwa kile kipengele"
Tuzo za Chaguo la Mteja Afrika 2022 (CCAA) ambazo zilianzishwa mwaka 2019 chini ya shirika la Lavine International Agency Limited na kwa mwaka 2022 zilizinduliwa June 7 jijini Dar es Salaam ambapo katika tuzo hizi washirika rasmi ni TANTRADE na Auditax International ambao ni mfumo wa upigaji kura unaothibitisha CCAA 2022
ZOEZI LA KUPIGA KURA TUZO ZA " CONSUMER CHOICE AWARDS" LAZINDULIWA RASMI
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 04, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 04, 2022
Rating:





Post a Comment