ASKOFU WA KKKT, DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI DOKTA MALASUSA ANATARAJIA KUONGOZA MKUTANO 36.
Na. Dominic Haule
Dayosisi ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) inatarajia kufanya Mkutano Mkuu wake wa 36 ambao Mkutano huo utafungualiwa na Mwenyekit na ambae pia Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dokta Alex Gehaz Malasusa utajumuisha wajumbe 424 ambao kati yao ni Wachungaji wote wa Dayosisi hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Msaidizi wa Askofu Bwana Chediel Lwiza wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, amesema kuwa Mkutano huo utafanyika kwa siku nne kuanzia Juma pili yaan Novemba 27 hadi 30 , 2022 katika Ushirika wa Mbezi Beach, Jijini Dar es salaam.
Bwana Lwiza amesema kuwa Mkutano huo hufanyika kila baada ya miaka miwili na ndiyo chombo kikuu Cha maamuzi ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Wakati huo huo amesema kuwa Miongoni mwa Mada zitakazo pewa kipaombele katika mkutano huo ni pamoja na kujadili Uteketezaji wa kazi mbalimbali zinazofanyika katika kipindi Cha miaka miwili iliyopita nakupanga Mipango ijayo kulingana na Mpango mkakati wa Dayosisi.
Pia amesema kuwa Mkutano huo Utajadili Maendeleo ya Dayosisi Katika nyanja ya kuhubiri Injili na huduma za jamii huduma za Afya, Elimu Makundi maalumu pamoja Mwenendo wa hali ya Kiuchumi kwa Ujumla.
Aidha amesema kuwa wajumbe Wengi watakao wakilisha mabara ya Wazee kutoka sharika 97 na Miata 208 Dayosisi Vituo vikiwemo Maendeleo ya Bank ,Upendo Media, Chuo kikuu Cha Tumaini Dar es salaam (TUDARCO) nk
Ameongeza kuwa Mkutano huo utaenda a na kufanyika Uchaguzi wa wenyeviti wa halimashauri za Idara na Bodi paomaja na Vituo na utaongozwa na Neno kuu la Mkutano wa Mwaka huu ni " Bwana Mmoja, Iman Moja , Ubatizo mmoja'. Waefeso 4:5
ASKOFU WA KKKT, DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI DOKTA MALASUSA ANATARAJIA KUONGOZA MKUTANO 36.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 25, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 25, 2022
Rating:

Post a Comment