HATI ZAIDI YA 200 ZATOLEWA UBUNGO, WANANCHI WAHOJI UJENZI WA KITUO CHA AFYA GOBA
BAADHI ya wananchi waliohudhuria kliniki iliyoandaliwa na Wizara ya Ardhi wamehoji uwepo wa mraji wa kituo cha afya katika Mtaa wa Tegeta A Manispaa ya Ubungo bila kushirikisha wananchi, wakizungumza na waandishi wa habari katika Mtaa wa Saranga wakazi hao wamesema uwepo wa ujenzi katika eneo hilo ni jambo jema lakini lazima hatua za kisheria zifuatwe kabla ya ujenzi kuendelea, hatua moja wapo ni uhalali wa eneo hilo ambalo lina migogoro na baadhi ya wananchi wenyeji katika kiwanja hicho
Injinia Raphael Peter mkazi wa Goba amesema eneo tajwa lilishafika katika mahakama na kutolewa uamuzi lakini kuna nguvu kubwa inatumika kujenga kituo ili hali mradi una manufaa kwa wananchi wote, "eneo la mradi halijapimwa wala kupangwa matumizi ya huduma za jamii, pia serikali ioneshe namna ilivyolitwaa eneo hilo ili kuepusha hasara hapo mbeleni kutokana na madai mbalimbali ya wenyeji wanaolalamika, serikali ifike na kuitisha mkutano wa wazi katika eneo hilo ili kumaliza utata na kumalizia wodi ya wazazi" alisema mkazi huyo
Naye Magdalena Yunusi anasema uvamizi katika viwanja vya michezo kwa watoto na maeneo ya mashule imekuwa ni tabia endelevu kwa baadhi ya watu na kusababisha vijana kukosa maeneo rasmi ya michezo na kurudi kukaa vijiweni, hivyo ameiomba serikali kuingilia kati uvamizi wa shule ya Matosa pamoja na eneo la Simba Oil ambalo awali ulikuwa uwanja wa kuchezea michezo
Mkuu wa idara ya Mipango miji Fadhiri Hussein amesema maeneo mengi yamesha tambuliwa na changamoto bado zinafika ofisi za Manispaa ili kutatuliwa, lakini kwa sasa vipande vingi vya Ardhi vimeshapimwa na wananchi wanachelewa kuchukua Hati kutokana kukosa viambatanisho muhimu, na mpaka sasa Hati 200 ziko tayari kutolewa
Fadhili amesema wananchi wenye maombi ya Hati baada ya kupimiwa wanapaswa kuja na namba za NIDA ambazo zinasaidia uwepo wa taarifa muhimu katika milki ya mtu, "kila mwananchi mwenye Hati anapaswa kuja na kitambulisho au namba za NIDA ili kurahisisha zoezi letu la kurasimisha vipande vya Ardhi katika manispaa ya Ubungo
Aidha mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Saranga Godwin Muro amekemea baadhi ya wenyeviti kujiingiza katika mauziano ya viwanja na kuchafua taswira nzuri za wenyeviti kwa kudai pesa za asilimia kumi huku wakijua ni kinyume na taratibu za mauziano, serikali kupitia Wizara ya Ardhi ilishaelekeza majukumu ya wenyeviti katika mauziano yatasalia kwenye kuwatambulisha wakazi wetu kwa wenye mamlaka ya kusimamia manunuzi lakini si kuwa sehemu ya manunuzi au kulazimisha wananchi kutoa fedha
HATI ZAIDI YA 200 ZATOLEWA UBUNGO, WANANCHI WAHOJI UJENZI WA KITUO CHA AFYA GOBA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 06, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 06, 2022
Rating:

Post a Comment