WAZIRI MKENDA ATOA WITO KWA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA MMONYOKO WA MAADILI
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, akitunuku vyeti kwa wanafunzi katika Mahafali ya Shule za Kiislamu za Ilala Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika leo Novemba 6,2022 katika uwanja wa Garden jijini Dar es Salaam.
Na Yusuph Digossi-Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, ametoa wito kwa viongozi wa dini kushirikiana na wamiliki wa shule na walimu kusimamia malezi ya vijana huku akikemea suala la mmonyoko wa maadili shuleni.
Waziri Mkenda ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam, kwenye Mahafali ya Shule za Kiislamu za Ilala Mkoa wa Dar es Salaam, yaliyofanyika katika uwanja wa Garden jijini humo.
" tumieni bidii zote kuhakikisha suala la mmonyoko wa maadili liwe muhimu na ninalaani vikali sana wale walioruhusu ule mchezo katika shule ile na mtu kurekodi video" amesema Waziri Mkenda.
Ameongeza kuwa ni lazima kuhakikisha wanafunzi wanapatiwa malezi bora kutoka kwa wazazi pindi wanapokuwa nyumbani na walimu wakati wakiwa shule ili kuepukana na mmomonyoko wa maadili.
Katika hatua nyingine Mkenda, amesema Serikali kupitia Wizara ya elimu italipa msukumo somo lenye kombinesheni kiarabu ili lifundishwe kidato cha tano na cha sita kwa sababu itasaidia kuzalisha wataalam wataokwenda kutafsiri kiarabu na kiswahili kwa kuwa ni lugha kubwa inayotumika umoja wa mataifa.
"Huu mjadala wa masomo ya dini kufundishwa shuleni tuliache kwanza, kwamba mtu anapochukua somo la dini liwe katika masomo yanayohesabika kuna sababu kadhaa lazima tuzizingatie hivyo siwezi kulizungumzia kwa sasa”
Kwa upande wake Shekh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amewataka watanzania na wadau wa elimu nchini kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya elimu nchini
WAZIRI MKENDA ATOA WITO KWA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA MMONYOKO WA MAADILI
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 07, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 07, 2022
Rating:




Post a Comment