MABADILIKO YA SHERIA WADAU WA HABARI WAUNGANISHA NGUVU , TEF CORI WAKUTANA NA JERRY SLAA
Kuelekea mabadiliko ya sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 wadau wa habari kupitia taasisi zote za habari wameendelea kuungana kwa lengo la kuwa na kauli moja na kufanya uchechemuzi kwenye mabadiliko ya sheria hiyo na kufikia lengo.
Hayo yamejiri Novemba 08 Jijini Dodoma wakati wa mkutano cha uongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF , Wadau wa Haki ya Kupata Habari (CoRI), na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jerry Silaa kilichokua na lengo la kumpitisha Mbunge huyo kwenye baadhi ya vifungu vya sheria ya habari ambayo vimekua vikilalamikiwa na wadau.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyiwa nje ya viwanja vya bunge Mwenyeki wa TEF Deodatus Balile amesema ndani ya sheria hiyo kuna vipengele mbalimbali kwa undani wake, vinaua tasnia ya habari akitolea mfano kipengele kinachompa nguvu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo kufungia chombo cha habari kwa namna anavyoona inafaa.
‘‘Katika safari ya mabadiliko haya, tumeungana taasisi zote za habari ili kuwa na kauli moja. Tumeunganisha nguvu ili kufikia lengo ’ amesema
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ukonga Dar es Salaam Jerry Silaa ameahidi kushirikiana na wabunge wenzake katika kuhakikisha tasnia ya habari inakuwa na sheria rafiki zinazotekelezeka.
‘‘Mimi na wabunge wenzangu tutashirikiana. Dunia imebadilika na hatuwezi kubaki hapa tulipo,’ alisema Jerry na kuongeza ‘‘nitazungumza na wenzange na kisha tutaona namna ya kufanya.’’
James Marenga, Mjumbe wa CoRI kutoka Taasisi ya Vyombo ya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania alimweleza Jerry kuwa tasnia ya habari ni kama tasnia nyingine nchini katia utendaji kazi.
‘‘Mimi ni mwanasheria, katika taasisi yetu tulitengeneza cord of conduct wenyewe na hizo ndio zinatuongozi, ni busara na wanahabari wakawa na utaratibu wao kisheria unaosimamiwa na wenyewe katika kuhakikisha maadili ya uandishi wa habari yanafuatwa,’’ alisema.
Naye Jessy Kwayu, Mkurugenzi Mkuu wa Media Brains Inc Ltd alisema, sheria ya habari ya mwaka 2016 ilipitishwa katia mazingira ambayo si rafiki.
MABADILIKO YA SHERIA WADAU WA HABARI WAUNGANISHA NGUVU , TEF CORI WAKUTANA NA JERRY SLAA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 08, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
November 08, 2022
Rating:




Post a Comment