Header AD

header ads

UTEKELEZAJI WA MKUMBI WAPUNGUZA TOZO , ADA NA FAINI 232



Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema Utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (MKUMBI) umefanikiwa ufutaji na upunguzaji wa tozo, ada na faini 232 na  kupitia na kurekebisha Sheria 40 zilizokuwa zinaleta changamoto katika ufanyaji biashara na uwekezaji nchini. 

Dkt. Kijaji ameyasema hayo wakati akifungua Semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari, Waandishi wa Habari pamoja na Watengeneza Vipindi vya uwekezaji, viwanda na biashara iliyolenga kutoa elimu kuhusu Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini ( MKUMBI) iliuofanyika Novemba 7, 2022 JNICC Dar es Salaam. 



Aidha amesema utekelezaji wa MKUMBI pia umefanikiwa  kuondoa urudufu wa majukumu na kuunganisha taasisi zenye majukumu yanayoingiliana kama TBS na TMDA,  kuanzisha mifumo ya Tehama, kuimarisha vituo vya utoaji huduma za mahali pamoja kama TIC na  kuanzishawa dirisha moja la kielektroniki la utoaji huduma kwa wawekezaji.  

Akiongea na washiriki hao, Dkt. Kijaji ameelezea misingi 10 inayopaswa kuzingatiwa katika utekelezaji wa MKUMBI inayolenga kuboresha utendaji kazi na utoaji huduma kwa umma kwa uwazi, kufanya maamuzi kwa mujibu wa sheria na kuongeza uwajibikaji katika sekta ya umma pamoja na kuimarisha majadiliano na ushirikishaji wa sekta binafsi. 

Ametaja misingi hiyo kuwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa Maboresho yanayofanywa na mamlaka za udhibiti yasilenge kuongeza mapato bali kukidhi gharama za utoaji huduma, Ukusanyaji wa mapato utumie nyezo rahisi na rafiki kwa kuweka vituo vya pamoja vya huduma au kuunganisha mifumo na  Kuondoa mwingiliano wa majukumu ya taasisi na  kuunganisha majukumu yanayofanana . 


Misinging mingine ni kuhakikisha  Sheria, Kanuni na Taratibu zinatekeleza sera ya biashara, ushindani, kumlinda mlaji na huduma za umma; Udhibiti uwe kwa lengo la kuendeleza sekta husika au uzalishaji; Kukuza ushindani wa kimkakati wenye usawa, tija na ubunifu, kwa kupunguza tozo na ada; Kuwa na mifumo ya udhibiti yenye uhakika, endelevu na inayotabirika;  Kanuni zote zitakazotungwa zifanyiwe tathmini ya athari ya udhibiti kabla ya kuidhinishwa kutumika; Kuhakikisha kuwa maboresho ya kupunguza kanuni hayaondoi mamlaka
UTEKELEZAJI WA MKUMBI WAPUNGUZA TOZO , ADA NA FAINI 232 UTEKELEZAJI WA MKUMBI WAPUNGUZA TOZO , ADA NA FAINI 232 Reviewed by Fahadi Msuya on November 08, 2022 Rating: 5