Header AD

header ads

MAOFISA UHAMIAJI WALIOFANYA UFISADI VIWANJA VYA NDEGE KUCHULIWA HATUA



NA HADIJA BAGASHA TANGA, 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani Injinia Hamad Masauni, amesema atawachukulia hatua maofisa Uhamiaji waliotajwa katika tume iliyoundwa kuchunguza ufisadi katika maeneo ya viwanja vya ndege.

Akifunga mafunzo ya maofisa uhamiaji katika chuo cha Uhamiaji Raphael Kubaga,  waziri alisema tume hiyo iliundwa kufuatia agizo la Rais Samia Suluhu Hassain alilolitoa wakati akizindua chuo hicho mapema mwaka huu ambapo alisema kuna maofisa uhamiaji katika viwanja vya ndege vya Zanzibar, Dar es salaam na Kilimanjaro,  wamekuwa wakiweka mifukoni fedha za malipo ya pasport badala ya kuingia serikali.


"Mheshimiwa Rais alipokuja hapa kuzindua chuo hiki, kuna mambo alielekeza ya kuyafanya, mapendekezo yoyote ya tume kuhusu askari aliyetajwa nitachukua hatua, hawatapona, " alisema waziri huyo. 

Waziri alisema tume hiyo ambayo mwenyekiti wake ni yeye,  katika mapendekezo yatakayotaja na ikithibitika askari wamehusika katika vitendo hivyo vilivyotajwa na Rais,  watachukuliwa hatua. 

Suala jiningine ambalo Waziri alisema katika utaratibu wa Rais wa kuviongezea  uwezo vyombo vyake vya ulinzi na usalama, wizara hiyo imetenga kiasi cha shilingi bilioni 5.6 kwa ajili ya kununua magari 32 ya jeshi la Uhamiaji mbapo gari moja litaletwa katika chuo hicho. 

Alisema changamoto zilizojitokeza kipindi Rais alipofika katika hicho, kama wizara wameweza kuyatatua ikiwemo kuchukua hatua kwa askari ambao wamekuwa wakikiuka maadili ya kazi zao. 


Alisema pia baada ya malalamiko mengi ya askari kukatwa posho zao (lation Allawance) katika bajeti imetengwa bilioni 16 katika fedha hizo Uhamiaji watapata shilingi milioni 900 ambazo maofisa waliomaliza kozi hiyo hawakukatwa hata senti moja. 

Alisema Rais Samia ametoa kipaumbele katika mafunzo ya askari hatua ambayo Wizara inampongeza kwasababu askari wanapata fursa ya kujifunza na kutekeleza majukumu yao. 

Waziri aliliagiza jeshi la polisi kuhakikisha wanawakamata wahalifu wanaotumia vyombo vya moto badala ya kukamata vyombo vilivyotumika kwa uhalifu na kushindwa kuwakamata wahalifu wenyewe. 


Awali Mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba alitoa ushauri kwa wizara ya Mambo ya Ndani,  kwamba kuhakikisha wanawahamisha askari waliokaa muda mrefu katika eneo moja ikiwemo kuwahamisha viongozi wote watakaoshindwa kusimamia kazi zao. 

Alisema unapomuhamisha mkubwa wa mkoa huku ukiwaacha watendaji katika wilaya,  kiongozi mpya anaweza asifanye kazi kwa ufanisi kutokana na mazingira hayo. 

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa alisema vyombo vya ulinzi na usalama linajitahidi kudhibiti wimbi la uhamiaji haramu pamoja na biashara za magendo mkoani Tanga,  kwa kushirikiana. 

Alisema zipo changamoto za ongezeko la wahamiaji haramu pamoja na mawakala wao ambapo jumla ya wahamiaji haramu 167 wameweza kukamatwa kutoka nchi za Ethiopia,  Somalia, Kenya,  Burundi,  Misri,  China,  Ghana na Watanzania 4 ambao ni wasafirishaji wa wahamiaji hao. 


Awali akitoa salamu za Chama Chama Mapinduzi (CCM) Mwenyekiti mpya wa mkoa wa Tanga,  Rajabu Abdallahaman alisema wapo watu wanakereka kwa ajili ya kumsifia Rais,  kwamba anaupiga meingi. 

"Mheshimiwa Waziri wapo watu wanakereka sana kwa mheshimiwa Rais kuambiwa anaupiga mwingi, basi miye naomba nirekebishe kidogo,  Dkt Anna Makakala anaupiga mwingi, mheshimiwa Omari Mgumba anaupiga mwingi,  MaDC wetu wanaupiga mwingi na mheshimiwa Rais anaupiga mwingi sanaaaaa," alisema mwenyekiti huyo ambaye amekuwa akipendwa na wana-Tanga. 

MAOFISA UHAMIAJI WALIOFANYA UFISADI VIWANJA VYA NDEGE KUCHULIWA HATUA MAOFISA UHAMIAJI WALIOFANYA UFISADI VIWANJA VYA NDEGE KUCHULIWA HATUA Reviewed by Fahadi Msuya on November 29, 2022 Rating: 5