Header AD

header ads

SERIKALI YA AWAMU YA SITA INA NIA YA DHATI NA MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI: WAZIRI NAPE



Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, amewahakIkishia wadau wa habari kukamilisha mchakato wa mabadiliko ya sheria ya habari.

Nape  ameyasema hayo Kwenye kikao chake na wadau wa Haki ya Kupata Habari (CoRI), tarehe 21 Novemba 2022, jijini Dar es Salaam alisema, serikali imepokea maoni yao kuhusu marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari Na 12 ya 2016.

" Niwahakikishie kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, inayo nia ya dhati katika jambo hili. Nimekuja mwenyewe kuwasilikiliza na imani yangu ni kuona sekta inaendelea kukua” alisema.

Kikao hicho cha pili cha Wadau wa Kupata Habari (CoRI) na serikali cha kupitia mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya habari, kiliongozwa na Nape mwenyewe.

Kwa upande wake Deodatus Balile Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), amesema kuna ishara nzuri kuelekea mabadiliko ya sheria ya habari.
SERIKALI YA AWAMU YA SITA INA NIA YA DHATI NA MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI: WAZIRI NAPE SERIKALI YA AWAMU YA SITA INA NIA YA DHATI NA MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI: WAZIRI NAPE Reviewed by Fahadi Msuya on November 21, 2022 Rating: 5