Jamii yaaswa kuwa na utamaduni wa kusoma vitabu kuongeza maarifa
Watanzania wameshauriwa kuendelea kuwa na utamaduni wa kusoma vitabu ili kujiongezea uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Atupele Mwakibete ambaye alimuwakilisha waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye wakati wa uzinduzi wa kitabu cha uongozi kilichoandikwa na Violet Mordichai Jijini Dar es salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mwakibete amesema watu wengi waliofanikiwa wana wastani wa kusoma angalau kitabu kimoja kwa siku lakini hal hiyo ni tofauti kwa hapa nchini watanzania wengi hawana utamaduni wa kusoma vitabu.
Amesema ili uwe kiongozi bora lazima upende kusoma ili kuongeza maarifa mapya kila siku kwa elimu haina mwisho huku akisisitiza kuwa uongozi sio lazima upate nafasi serikalini bali unaanzia katika ngazi ya familia.
Kwa upande wake Violet MordichaI ambaye ni mtunzi wa kitabu hicho amesema kuwa anaamini watu watakaosoma kitabu hicho watapata maarifa ya kuwa viongozi bora watakaoleta mandeleo katika jamii.
Jamii yaaswa kuwa na utamaduni wa kusoma vitabu kuongeza maarifa
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 17, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 17, 2022
Rating:




Post a Comment