Serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kulegeza ugumu wa sekta ya habari
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amesema licha ya vyombo vya habari kuonekana kuwa huru, wadau wa sekta hiyo wanaamini kuwa uhuru zaidi utapatikana pale sheria ya huduma za vyombo vya habari itakapofanyiwa marekebisho.
Balile ameyasema hayo leo Desemba 17, 2022 wakati wa kongamano la kwanza la maendeleo ya sekta ya habari linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema Serikali ya awamu ya sita imesadia kulegeza ugumu uliokuwa unaikabili sekta hiyo na kuvifanya vyombo vya habari kutokuwa huru.
“Kuna wakati sheria kwenye sekta ya habari zilikuwa kitanzi magazeti yalifungiwa na uhuru ukapotea kabisa, ilivyokuja Serikali ya awamu ya sita, yamefanyika maboresho makubwa. Rais aliondoa mtanziko uliokuwepo, sasa hivi tuna raha kwa kweli.
“Hata hivyo tunaamini utulivu huu tuliona utalinda kisheria baada ya kufanyiwa kwa marekebisho ya sheria ya huduma za habari kama ambavyo tumeahidiwa,” amesema Balile.
Serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kulegeza ugumu wa sekta ya habari
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 17, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 17, 2022
Rating:


Post a Comment