MKENDA ARIDHISHWA NA KIWANDA DARASA DIT
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza vipuri vya vyombo vya moto unaofanywa na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).
Waziri ametembelea kiwanda hicho cha kujifunzia leo kuona hatua iliyofikiwa. Kiwanda hicho kinatarajiwa kufunguliwa rasmi kitakapo kamilika.
Prof. Mkenda ameridhishwa na uwekezaji na maboresho yaliyofanyika ambapo amesema kuna mabadiliko mengi mazuri yamefanyika tofauti na alipotembelea mwezi julai.
"Nimeridhishwa na uboreshaji ulifanyika mpaka sasa, kutoka kwenye utengenezaji wa Vipuri vya bajaji pekee mpaka vipuri vya magari hongereni sana hii ni hatua nzuri," amesema.
Prof. Mkenda amesisitiza kuwa DIT kupitia kampuni Tanzu ya taasisi hiyo (DIT Company Ltd) ifuate taratibu zote ili kuhakikisha hatimiliki inapatikana kwa ajili ya kazi ya uzalishaji inayofanywa kupuka bunifu hizo kuibiwa.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi, Mhandisi Dkt. Richard Masika amesema pamoja na kutengeneza vipuri, DIT inatarajia kutengeneza na kuuza mashine za kutengenezea vipuri ili kuweza kukidhi mahitaji ya soko.
MKENDA ARIDHISHWA NA KIWANDA DARASA DIT
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 02, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 02, 2022
Rating:




Post a Comment