Header AD

header ads

RAIS DKT SAMIA: TANZANIA INAWEZA KUFANYA MAMBO MAKUBWA



Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema mradi wa Bwawa la Nyerere unatoa ujumbe duniani kwamba Tanzania inaweza kutekeleza mambo makubwa yakuweza hata kubadilisha taswira yake.

Dkt. Samia amebainisha hayo leo Desemba 22, 2022 mkoani Pwani akizungumza katika hafla ya ujazaji maji katika Bwawa hilo, mradi ambao ukikamilika utazalisha Megawati 2115 za umeme.

“Mradi huu unatoa ujumbe Duniani kwamba Tanzania inaweza kutekeleza mambo makubwa ya kuweza kubadilisha hata taswira yake na ya ulimwengu kwani Bwawa hili linaonekana kutoka anga za juu kabisa na kuweza kuwa na alama katika ramani mpya ya Dunia,” amesema Rais Dkt. Samia.

Rais Dkt. Samia amesema mradi huu utaipatia Tanzania umeme wa uhakika kwa ajili ya maendeleo endelevu na kutimiza ndoto iliyokuwepo tangy zamani kutokana na fikra za viongozi waliopita mwanzilishi akiwa ni Hayati Mwal. Julius Nyerere Rais wa Awamu ya Kwanza.
RAIS DKT SAMIA: TANZANIA INAWEZA KUFANYA MAMBO MAKUBWA RAIS DKT SAMIA: TANZANIA INAWEZA KUFANYA MAMBO MAKUBWA Reviewed by Fahadi Msuya on December 22, 2022 Rating: 5