Header AD

header ads

MZEE MWINYI KUSHUHUDIA UJAZAJI WA MAJI KWENYE BWAWA LA NYERERE



Rais mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na  Samel Shokry Waziri wa Mambo ya nje wa Serikali ya Misri ambaye ameiwakilisha Serikali nchi hiyo Katika zoezi la uzinduzi wa ujazaji wa maji Katika bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere JNHPP ambaoo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  Samia Suluhu Hassan atashuhudia



Wakuu wa mashirika mbalimbali ya kimataifa wakiwa Katika hafla hiyo inayofanyika Leo kwenye mradi WA bwawa la umeme la Julius Nyerere JNHPP.

Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria Katika uzinduzi huo wa kukaza maji kwenye bwawa la Julius Nyerere JNHPP Leo Kushoto ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.

Na Mwandishi Wetu, Rufiji

MAELFU ya wananchi wa mikoa ya Pwani, Morogoro na Dar es Salaam wamejitokeza katika zoezi la kuanza ujazaji wa maji kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP), lililopo wilayani Rufiji mkoani Pwani.

Zoezi hilo la ujazaji maji linazinduliwa leo na Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye ameambatana na viongozi mbalimbali wa serikali na kisiasa.

Bwawa hilo ambalo ujenzi wake umegharimu Sh.trilioni 6.5 linatarajiwa kuzalisha megawati za umeme 2,115 ambazo zitaingizwa kwenye gridi ya taifa na kumaliza changamoto ya umeme nchini.

Mwitikio wa wananchi zaidi ya 2,000 katika tukio hilo la ujazaji maji unatokana umuhimu wa mradi huo kwa maendeleo ya nchi kwa miaka ijayo.

Mradi huo ulianza kujengwa kupitia Serikali ya Awamu ya Tano ambayo ilikuwa ikiongozwa na Rais John Magufuli ambapo Rais Samia ameendeleza na leo atazindua zoezi la ujazaji maji.

Kwa mujibu wa Waziri wa Nishati, January Makamba mradi huo umefikia asilimia 78 ya ujenzi na unatarajiwa kukamilika 2024.

Mradi huu wa JNHPP ambao utazalisha megawati 2,115 utakuwa mkubwa kwa Afrika Mashariki na wanne kwa Afrika.

Akifafanua kuhusu ujenzi wa mradi huo Mhandisi Said Kimbanga alisema kuna mitambo tisa ambapo kila mmoja utakuwa unazalisha megawati 235, hivyo kwa jumla kuzalisha megawati 2,115.

Amesema maji ambayo yataingia kuzalisha umeme yanatoka Mto Kilombero, Ruaha Mkuu na Kuwegu.

Mhandisi Kimbanga amesema eneo la mradi bwawa huo lina ukubwa wa hekta 915 ukubwa ambao ni sawa na ziwa ambapo ujazo wa maji lita bilioni 32.
MZEE MWINYI KUSHUHUDIA UJAZAJI WA MAJI KWENYE BWAWA LA NYERERE MZEE MWINYI KUSHUHUDIA UJAZAJI WA MAJI KWENYE BWAWA LA NYERERE Reviewed by Fahadi Msuya on December 22, 2022 Rating: 5