SERIKALI YAPONGEZWA MCHAKATO WA MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI YA MWAKA 2016
Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Deogratius Nsokolo amesema, Rais Samia Suluhu Hassan tangu alipoingia madarakani, ni rafiki wa waandishi wa habari.
Akizungumza wakati akitoa maoni yake leo kuhusu mwenendo wa mchakato wa mabadiliko ya sheria ya habari nchini, ameeleza maendeleo ya mchakato huo yanatokana na kuridhiwa na Serikali ya Rais Samia.
“Rais Samia tangu alipoingia madarakani, alikuwa karibu na sekta ya habari na kutoa matumaini ya kufanyiwa marejeo kwa sheria hi ya mwaka 2016. Na tayari matokeo yake ni wadau wa habari na serikali kukaa kwa pamoja na kuainisha vipengele gani tungependa viondolewe,” alisema.
Amefafanua , kazi iliyobaki sasa ni upande wa serikali kukamilisha mchakato na kisha mapendekezo hayo kupelekwa bungeni kwa mujibu wa sheria za nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, alisema mchakato huu unakwenda kwa kuwa, rais aliyepo madarakani ana dhamira njema na sekta ya habari.
SERIKALI YAPONGEZWA MCHAKATO WA MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI YA MWAKA 2016
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 14, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 14, 2022
Rating:


Post a Comment