VIJIJI ZAIDI YA ELFU 12 TANZANIA BARA KUPATA HUDUMA YA UMEME KUPITIA REA
Hayo yamesemwa leo Alhamisi Desemba 8, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy wakati akieleza kuhusu mafanikio ya REA kwenye miradi ya kusambaza nishati vijijini akiwa kwenye ujenzi wa Kituo cha kupoza umeme Ifakara
Pia Mkurugenzi Mkuu huyo amesema katika kuendeleza dhamira ya Serikali kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma ya umeme kwa mwaka huu wa fedha wakala huo unatarajia kuanzisha mradi wa ujazilizi awamu ya pili B na awamu ya Pili C.
Amesema mradi wa ujazilizi awamu ya Pili B utapeleka umeme katika vitongoji 1600 kwenye mikoa 9 huku mradi wa ujazilizi amamu ya pili C ukitarajiwa kupeleka umeme katika vitongoji 1800 kwenye Mikoa 11 .
VIJIJI ZAIDI YA ELFU 12 TANZANIA BARA KUPATA HUDUMA YA UMEME KUPITIA REA
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 08, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 08, 2022
Rating:

Post a Comment