Serikali kuikabidhi NIT ndege mbili za mafunzo ya urubani
Mkurugenzi wa uthibiti wa Barabara, Eng Johansen Kahatano amekipongeza Chuo cha taifa cha Usafirishaji(NIT) kwa mageuzi ambayo wameyafanya kwa kupanua wigo wa mitaala na kufikia maeneo mengi ya usafirishaji ikiwemo, barabara, reli , anga, maji na bomba
Ameyasema hayo leo Disemba 8 katika kongamano la 9 la kuwapongeza wahitimu wa chuo cha NIT waliofanya vizuri katika masomo ya nadharia na vitendo katika chuo cha Taifa cha usafirishaji.
Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha usafiri, Dkt Prosper Mgaya amesema kongamano hilo linawaunganisha wanafunzi waliomaliza mwaka huu na kwenda kuwaunganisha ma wenzeo ambao walishamaliza NIT na kuingia kwenye umoja ambao wa wanafunzi waliomaliza chuo cha taifa cha usafirishaji.
Amesema kuwa mwaka huu chuo cha NIT kimejikita kwenye usafiri wa reli kwa sababu serikali inawekeza fedha katika usafiri wa reli.
Pia amesema kwa upande wa usafiri wa Anga wanategemea ndege mbili za mafunzo ya urubani kukabidhiwa na serikali hivi karibuni.
Serikali kuikabidhi NIT ndege mbili za mafunzo ya urubani
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 08, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 08, 2022
Rating:


Post a Comment