Watetezi wa haki za binadamu watakiwa kuungana kwa pamoja
Watetezi wa Haki za binadamu wametakiwa kuungana kuwa na sauti ya pamoja kutetea haki za binadamu hasa katika kukemea uvunjifu wa haki hizo ili kila mwenye haki aweze kupata haki yake stahiki.
Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam, Mshauri wa Mambo ya Kisheria KKKT- Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Manford Kijalo, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi rasmi wa kampeni ya Masuala ya haki za binadamu na hasa kwa Tanzania katika suala zima la kumiliki na kutumia ardhi iliyoanzishwa na Jumuiya ya kimataifa (UEM).
"Kwetu hapa Tanzania utetezi wa haki za binadamu utajielekeza katika wahanga wa matatizo ya viwanja /ardhi kwani migogoro imekuwa ni mingi sana"
"Haki za binadamu zinatambuliwa ulimwenguni kote, ni misingi ya maadili inayotakiwa kutumika kwa manufaa ya binadamu wote duniani na kwa usawa" Aliongeza Mchungaji Kijalo
Mchungaji Kijalo alisema kwa Tanzania kumekuwa na matatizo mengi na migogoro mingi katika suala zima la umiliki na matumizi ya viwanja/ardhi hasa pale ambapo wahanga alipopoteza ardhi zao kwa njia ya hila kutoka kwa baadhi ya watendaji wakishirikiana na watu wenye fedha.
"Jamii yetu ya kitanzania inategemea sana ardhi kwaajili ya kuendesha maisha yao, mfano kilimo, ujenzi wa nyumba na uwekezaji mwingine wowote hivyo sisi na UEM tuna wajibu wa kusimama na hawa wahanga ili kuona ni jinsi gani wanaweza kuinuka na kubaki katika furaha na amani ya matumizi ya ardhi katika nchi yao "
Kijalo aliongeza kuwa kilichoisukuma jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kunakuwa na mifumo thabiti ya ulinzi wa haki za binadamu ni mateso na uhalifu mkubwa dhidi ya binadamu uliofanyika wakati wa vita ya pili vya Dunia vilivyoanza tarehe 1 Septemba 1939 na kumalizika tarehe 2 Septemba 1945.
Mchungaji Kijalo alisema Msingi wa haki za binadamu katika biblia kutoka kitabu cha Mwanzo 1:27 inasema kuwa 'Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu aliwaumba, Mwanamume na Mwanamke aliwaumba '
Pia Mchungaji Kijalo alisema wataendelea kutoa elimu kupitia vipindi mbalimbali vya Televisheni kuhusu sheria za kupata na kumiliki viwanja, wajibu wa serikali katika masuala ya ardhi na wajibu wa kanisa katika kutatua migogoro ya ardhi
Watetezi wa haki za binadamu watakiwa kuungana kwa pamoja
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 21, 2022
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
December 21, 2022
Rating:



Post a Comment