Header AD

header ads

Diwani Lyoto :Vijana kata yangu ya Mzimuni wataleiewa kisoka Ng'ambo



Diwani wa kata ya Mzimuni, Magomeni Manfred Lyato ambaye ni mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam amesema michezo ni ajira ambayo ilitumika kwa vijana inaweza kuwatoa kimaisha.

Hayo yamesemwa juzi na Lyato akipambanua mambo ya maendeleo katika kata yake hiyo Jijini humo.

Amesema vijana wakiandaliwa vyema katika medani ya kimichezo wanaweza kuilete sifa nchi sambamba na kukuza kipato chao.

" Nilipanga kuwapeleka takribani vijana wa nne kwenda kulelewa kimichezo katika shule za kimichezo nchini China lakini ilishindikana kutokana na janga la UVIKO 19 ambapo liliweza kuvuruga mipango yote hiyo niliyokuwa nimelenga kuwapatia mafunzo nchini humo,"amesema Mhe.Lyato.

Mbali na malengo hayo kutotimia kwa sasa nipo katika mipango mingine ya kimkakati kuhakikisha malengo ya mapya katika kukuza vipaji sahihi yanatimia kwani nimejipanga upya .

Amesema kwa sasa nimeanza kujipanga ambapo namaono ya kuwapeleka vijana wengine nje ya nchi huku akiitaja nchi ya Swiden kama sehemu moja wapo ambayo imekuwa ikichangia kuonekana haraka kwa vijana wanaopitia hapo kisoka kwenda nchi zingine zilizo endelea kisoka.
Diwani Lyoto :Vijana kata yangu ya Mzimuni wataleiewa kisoka Ng'ambo Diwani Lyoto :Vijana kata yangu ya Mzimuni wataleiewa kisoka Ng'ambo Reviewed by Fahadi Msuya on January 18, 2023 Rating: 5