Meneja mrema wa Soko la Kimataifa la Samaki Feri Apania Kukuza Mapato Kimkakati
viongozi wao wa wadau wa soko kuhakikisha wanawasilisha kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala, majina ya watu wote wanaotaka mikopo.
Ata hiyvyo amesema kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wafanyabishara lakini wanaendelea kujitahidi kuhakikisha suala la usafi wa soko unafanyika ipasavyo ili kuzuia Magonjwa ya mlipuko ambapo kuna gari taka linalotoa huduma kila wakati ,nakwamba changamoto iliyopo ni upatikanaji wa mipira,magadi, sabuni,blashi, gloves,mifagio,pamoja na matoroli ili kuifanya kazi ya mzabuni wa taka sokoni hapo kuwa nyepesi nakuhakikisha usafi unafanyika Kwa kiwango kinachotakiwa.
“Soko hili limekuwa likijiendesha kupitia mapato tunayokusanya,mimi na vijana ninaosaidiana nao kukusanya ushuru tunaangalia na kujiwekea malengo ya kukusanya kwa mwaka na kugawanya kwa miezi 12 kila mwezi tukusanye kiasi gani, hivyo tunahakikisha pia kila mwisho wa mwezi tunapeleka asilimia 30 ya mapato katika halmashauri Kwa ajili ya shughuli za maendeleo,na hatujawahi kuacha kupeleka “amesema Mrema.
Amesema kuwa soko hilo limefanikiwa kuongeza kina cha maji na kuzifanya boti za uvuvi kufanya kazi yake vizuri,pia soko hilo linatarajia kujenga jengo kubwa la kisasa kwa ajili ya kupumzika wavuvi wanapotoka baharini kuvua samaki ambapo tayari tenda ya kutafuta mzabuni imeshatangazwa na Halmashauri ya Manisapaa ya Ilala,nakwamba pia halmashauri hiyo mwishoni mwa mwaka 2022 imepeleka sokoni hapo injini ya boti inayofanya doria na kulinda mazao ya baharini.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabishara wa soko hilo Tausi Isaya ambaye ni mamalishe na Obed Samueli ambaye ni baba lishe katika soko hilo,kwa nyakati tofauti wamesema kuwa mfumuko wa bei ya vyakula uliopo kwa sasa unasabbisha wasipate faida kwenye biashara wanazofanya, nakwamba pia kuna baadhi ya Wafanyabiashara wa chakula kutoka nje ya soko wanakuja kufanyabiashara ndani ya soko hilo hali inayochangia pia wafanye biashara katika mazingira magumu.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
January 17, 2023
Rating:


Post a Comment