Mhe.Lyoto : Apongezwa kwa kutekeleza Ilani ya CCM kwa Vitendo Kata ya Mzimuni
Diwani kata ya Mzimuni wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam, Manfred Lyato amepongezwa na kamati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata hiyo kwa kujitolea kuwalipa posho watumishi wa afya wanaojitolea katika Zahanati ya Mzimuni.
Mhe.Lyato amepongezwa kwa kuweza kuwa kichocheo cha maendeleo katika kata hiyo kwa kutoa jumla ya Sh.Mil.1 ambapo kila mwezi imeweza kuwalipa posho watumishi hao wa afya.
Mbali na kujitolea huko kamati hiyo ya siasa imemsifia kwa kuweza kutimiza Ilani ya (CCM) kwa kuweza kutoa mikopo ya Sh.Mil.154 kwa kina mama ,vijana na watu wenye mahitaji maalum ambayo utolewa na halimashauri .
Akizungumzia mipango ya kimkakati ya kata hiyo Lyato amesema ameisha jitolea pia kuchangia Bima ya Afya kwa kwa wazee 20 yenye dhamani ya Sh.800,000 , sambamba na kuchangia Sh.Mil.1.4 katika kufanikisha ujenzi wa choo cha Zahanati ya kata hiyo ambayo ilitumika kununua baadhi ya vifaa vya ujenzi.
"Mwezi ujao nitaweza kufanya mikakati mingine ya maendeleo kwani takuwa nimeanzisha foundation itakayo weza kuisaidia kata yangu katika wigo Mpana,"amesema Lyato.
Mhe.Lyoto : Apongezwa kwa kutekeleza Ilani ya CCM kwa Vitendo Kata ya Mzimuni
Reviewed by Fahadi Msuya
on
January 13, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
January 13, 2023
Rating:

Post a Comment