TAASISI YA MOI YAFANYA JAMBO HILI KUBWA LEO.
NA KAROLI VINSENT
katika kuonesha wanaongeza ufanisi kazini TAASISI ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imeanza kutoa mafunzo ya mwaka mmoja kwa wataalmu wake ambapo wagonjwa 40 watafanyiwa upasuaji wa kisasa wa kutoa damu iliyovuja katika ubongo na kuziba mishipa .
Hata hivyo,Moi imesema katika mafunzo hayo wataalmu watatu watafundishwa njia ya haraka ya kutoa damu na kuziba mishipa iliyopasuka kutokana na mgonjwa kupata stroke.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa MOI ,Dk Respisius Boniface wakati akizungumza na waandishi wa habari,amesema wanapata ongezeko la wagonjwa waliopasuka mishipa ya damu kwenye ubongo na husababishwa na presha.
Hata hivyo,Dkt Boniface Ameeleza kuwa Kwa wiki wanaapata wagonjwa waliopasuka mishipa ya damu kichwani na damu kuvuja katika ubongo saba mpaka 10 na kwa mwaka 120 hadi 150.
"Kila siku wataalamu wanazungumza magonjwa yasiyoambukiza yanaongezeka kwa kasi na wanahamasisha kuzuia kubadili stayle ya maisha yanaleta shida.
Ameongeza "Tumeona pamoja na kuzuia tujipange kuwatibu na tumeanzisha mafunzo maalum ili kusidia nchi yetu tutakuwa tunafundisha na tumenza na Prof Atanasi kutoka Ujeruma haya ni mafunzo endelevu.
Mtaalamu huyo ameongeza kuwa kwa Safari ya kwanza wamepanga kuwafanyia wagonjwa saba na hadi sasa wanne tayari hivyo watafundishwa njia ya kisasa.
"Sasa tumeanza na wataalamu wa MOI halafu baadae tutaenda na madaktari wa hospitali nyingine na tutafanya kwa mwaka mmoja,"amesisitiza.
Pamoja na hayo Dk Boniface amesema oparesheni hizo zina gharama ya Sh milioni nane hadi 12 na nje ya nchi Sh milioni 50 hadi 60 hivyo kwa kila mgonjwa kiasi cha Sh milioni 40 zimeokolewa.
"Presha zamani ilikuwa watu wazima miaka 55 hadi 60 lakini sasa tunapata vijana hadi miaka 35 kwasababu ya mabadiliko ya maisha na endapo mgonjwa akichelewa ubongo unakufa hata akifanyiwa matibabu hawezi kurudi kwenye hali ya kawaida,"ameeleza.
kwa upande wake Daktari Bingwa wa Ubongo,Uti w mgongo na Mishipa ya Fahamu ,Nasforas Rutabasigwa amesema kuwa Utaalamu unaongezeka hivyo wanatarajia kufanyia wagonjwa 40 kwa mwaka na kwa awamu nne watawafanyia wagonjwa 10 wataalamu wa ndani watakuwa na uwezo na wao pia watawafundisha wenzao.
"Moi kushirikiana na MUHAS tumeanzisha mafunzo kufundusha magonjwa ya mishipa ya damu tunafanya utaalamu kutoka kwa wenzetu ,Kwa vile namba ya wagonjwa inaongezeka na kwasababu kila mkoa kuna CT-Scan wagonjwa wanagundulika kama damu imevuja kwenye ubongo,"amefafanua.
Amesema Ugonjwa huo ni rahisi mgonjwa kupoteza maisha ndani ya wiki mbili.
"Kupitia mtaalamu huyo watafanya mafunzo kwa awamu ya kwanza alifanya mwenyewe na awamu ya pili atafanya nusu na wataalamu wetu watamalizia na awmu ya tatu na nne wataalmu wetu watafanya wenyewe.
Amesema kwasasa wana wataalamu 10 hadi 15 na wataalmu watatu wanaopata mafunzo wataenda nao mpaka mwisho na hao wtawafundisha wengine.,
TAASISI YA MOI YAFANYA JAMBO HILI KUBWA LEO.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
January 13, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
January 13, 2023
Rating:



Post a Comment