Header AD

header ads

MSHINDI WA CHOMOKA NA NDINGA YA PARIMATCH AKABIDHIWA GARI LAKE



Mkazi wa Lindi, Hamidu Mohamed Abdallah mwenye umri wa miaka 28 leo januari nne amekabidhiwa rasmi  gari yake aina ya Toyota Urban Cruiser yenye thamani ya shilling million 65 baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya chomoka na Ndinga kutoka Parimatch

promosheni hiyo iliyodumu kwa siku 35 kuanzia tarehe 22 Novemba hadi 26 Disemba 2022 iliwapa wateja nafasi ya kujishindia zawadi za simu mbili kila siku, bodaboda mbili kila mwisho wa wiki na droo ya mwisho mshindi alikuwa akijinyakulia zawadi ya gari mpya kabisa

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Parimatch Tanzania, Bwana Erick Gerald Wakati wa kukabidhi gari hilo kwa mshindi na kuwashukuru wateja wote ambao wameshiriki na baadhi yao kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo simu na bodaboda ambazo zilitolewa na kampuni hiyo 


"Tunayo furaha kubwa katika kipindi hiki cha mwaka mpya kumkabidhi mshindi wetu wa gari aina ya Toyota Urban Cruiser, gari hii ni jipya kabisa yaani zero kilomita. Tunawashukuru wateja wetu nchi nzima walioshiriki kwenye promosheni hii ya siku 35 ambayo imemalizika mwishoni mwa mwezi wa Disemba 2022" . amesema Gerald

Kwa upande wake mshindi wa gari hiyo, Hamidu Mohamed amewashukuru Parimatch Tanzania kwa kuweza kutimiza ndoto yake kumiliki gari kutoka katika kampeni ya chomoka na Ndinga

"Wakati napigiwa simu nilikuwa nyumbani nimelala maana siku hiyo kulikuwa na mvua kubwa sikuweza kuamini kaa haraka ila baadae nilipopigiwa tena na kupata ile taarifa kwamba nimeibuka mshindi nilifurahi sana kwani sikutegemea kabisa kuwa ningeibuka mshindi katika promosheni hii, jambo hili naloja kama ndoto kwangu", amesema Hamidu


Kwa upande mwingine kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa hofu kuwa ya bonasi ukaribisho ya 100% hadi kufikia Tanzania shilling 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nao

Parimatch imekuwepo nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual. Mbali na soka , kampuni ya Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, kriketi, na Michezo mingine mingi ya live na pre-match.
MSHINDI WA CHOMOKA NA NDINGA YA PARIMATCH AKABIDHIWA GARI LAKE MSHINDI WA CHOMOKA NA NDINGA YA PARIMATCH AKABIDHIWA GARI LAKE Reviewed by Fahadi Msuya on January 04, 2023 Rating: 5