UDP yaviomba Vyama Vya Siasa Kushirikiana.
Chama Cha United Democratic Party ( UDP) kimeviomba vyama vya siasa kuwa kitu kimoja nakuacha kubaguana kwani vyama hivyo vipo katika nia moja yakuwatetea wananchi.
Hayo yamesemwa Februari 17 2023 na Mwenyekiti Taifa wa Chama hicho Jonh Cheyo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam juu ya mambo matatu muhimu ikiwemo suala la madai ya Katiba Mpya,Ugumu wa Maisha pamoja na kuruhusiwa kwa Mikutano ya hadhara.
Cheyo amesema kuwa suala la Katiba mpya tayari Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo baada ya kupokea ripoti ya Kikosi kazi lakini bado baadhi ya vyama vya siasa vimekua vikijitokeza kuhoji huku suala hilo akidai kuwa ni lakitaifa hivyo linahitaji ushirikishwaji wa wananchi.
Katiba iliyopo imedumu miaka zaidi ya 60 hivyo ni agenda ya wananchi siyo ya vyama vya siasa Pekee,Kuna vyama vimekua vikijiona vikubwa nakuona vyama vyetu ni vidogo hivyo vyama hivi vitatuletea shida ,jambo la Katiba nila wananchi" amesema Cheyo.
Kuhusu Mikutano ya hadhara Mwenyekiti huyo amevitahadhalisha vyama vya siasa kufanya siasa za kistaarabu,kupendana huku akisisitiza kuwa endapo Chama hicho kitashika Dola kitahakikisha wananchi wenye ardhi wanamiliki ardhia yao kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
"Kuruhusiwa Kwa Mikutano ya hadhara ni jambo jema,hivyo tufanye siasa za kistaarabu,tuwaeleze wananchi sera zetu,tuache matusi ,ili tuwafanye wananchi watuelewe nakuweza kutuchagua Kuwaongoza" amesema Mwenyekiti huyo.
Akizungumzia kuhusu suala la Ugumu wa Maisha amesema kuwa Hali hiyo inasababishwa na kupanda Kwa gharama za nishati mafuta ya dizeli hivyo gharama za usafirishaji wa bidhaa zimepanda nakusababisha Hali ya ugumu wa Maisha.
" Namuomba Rais Dkt Samia atumie wafanyabiashara wenye Uwezo wa kuagiza mafuta ya dizeli kwa bei nafuu ili kuweza kupunguza gharama za mafuta ya dizeli nakuondoa gharama za usafirishaji hali itakayofanya Maisha kuwa rahisi.
"Hapa vinahitajika vitu viwili kwanza serikali isimamie ubora wa mafuta kupitia TBS ,pili bei ya mafuta pia isimamiwe vizuri na EWURA ,tukifanya hivi tutaweza kudhibiti malalamiko ya wananchi kuhusu ugumu wa Maisha"
UDP yaviomba Vyama Vya Siasa Kushirikiana.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
February 17, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
February 17, 2023
Rating:

Post a Comment