Header AD

header ads

Vijana watakiwa kuchangamkia fursa za uwekezaji Bagamoyo.



Dar es salaam, 

Na Emmanuel Kawau.

Kampuni ya Vijana Real Estate inayojihusisha na upimaji na uuzaji wa viwanja na mashamba hii leo rasmi imemtangaza maulid kitenge kuwa balozi wake.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo February 16/2023 mkurugenzi mtendaji wa Vijana Real Estate Campany Ltd Ndg Azaidu Daudi Mohamedi amesema wanaamini nguvu za vijana katika kufanya mabadiliko chanya kwenye jamii na wanategemea kuwa maulid kitenge atakwenda kuwa balozi mzuri na kuwaeleza vijana na jaamii kwa ujumla faida ya kutumia kampuni yao kuweza kumili kiwanja.


Aidha amesema vijana Real Estate inauzoefu wa miaka mitatu katika uuzaji wa viwanja ambapo wana mradi wa uuzaji viwanja mpiji magoe,mbweni,madale na sasa wapo kilomo Bagamoyo,Mkoani pwani.

"Tunauza viwanja vyenye ukubwa kuanzia square mita 450, na viwanja vyetu vimepimwa kabisa na ukinunua kiwanja kwetu utapatiwa na hati miliki na utakuwa na uwezo wa kulipa kidogo kidogo" Alisema Azaidu.

Kwa upande wake balozi wa Vijana Real Estate Campany Ltd Maulid kitenge amesema Mji wa Bagamoyo hivi sasa kumekucha na serikali hivi karibuni inatarajia kuanza mchakato wa bandari ya Bagamoyo ambayo ni kubwa Barani Afrika hivyo ukiwekeza katika mji huo manufaa yake ni makubwa hapo baadae.

Ameongeza kuwa mradi wa viwanja vya vijana realestate upo Kilometer 8 kutoka eneo itapojengwa bandari na pia upo Kilometer 4 kutoka barabara kuu.

" Tunawaita vijana kuja kuwekeza,vijana ndio wenye nguvu ya kuleta mabadiliko katika jamii kutoka sehemu moja kwenda nyingine,viwanja vyetu vimepimwa,vinahati,ni eneo la bambalale hakuna mabonde wala milima wito wangu kwenu jamii nzima ya kitanzania ni tuchangamkie fursa hiyo" Amesema kitenge.
Vijana watakiwa kuchangamkia fursa za uwekezaji Bagamoyo. Vijana watakiwa kuchangamkia fursa za uwekezaji Bagamoyo. Reviewed by Fahadi Msuya on February 17, 2023 Rating: 5