Header AD

header ads

Hospitali y rufaa Mkoa wa Tanga ina uhaba wa chupa 200 za damu




Na Hadija Bagasha Tanga, 

Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tanga ya Bombo ina uhaba wa chupa 200 za damu kwa mwezi jambo ambalo limekuwa likihatarisha maisha ya wagonjwa wanaopelekwa hospitalini hapo kwajili ya matibabu. 

Mkuu wa kitengo cha maabara katika hospitali hiyo dkt  Sinde Mtobu amesema wanapopewa rufaa wagonjwa ya kwenda kwenye hospitali hiyo wakitokea kwenye wilaya mbalimbali Mkoani humo wakati mwingine wanakutana na changamoto hiyo ambayo inawafanya madaktari kujikuta wakiwa katika wakati mgumu wa kuokoa maisha ya mgonjwa. 


Alisema uhitaji wa damu kwa mwezi katika hospital hiyo ni mkubwa tofauti na ile inayochangiwa ambapo uhitaji wao  unafikia lita 500 hadi 600 wakiwa na upungufu wa damu kwa chupa 250 hadi 300 hivyo kuziomba taasisi na watu binafsi kuona umuhimu wa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu.

"Tunashukuru  sana siku ya leo tupo na wenzetu wa taasisi ya Bilal Muslim ambao kila mwaka huwa wanakuja kuchangia damu salama kwaajili ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu tunawashukuru sana kwasababu kila mwaka wana tukio kama hili tunawapongeza kwa moyo wao huo wa kuweka katika kalenda yao" alisema Mtobu.


" Sisi kama hospital kwa wastani kwa mwezi tunatumia  chupa za damu 500 mpaka 600 lakini uwezo wa kuchangia damu ambayo inapatikana  mara nyingi  tunapata unit 250 mpaka 300 kwahiyo uhitaji wa damu kwa wagonjwa ni mkubwa ,  kikubwa niiase jamii kwa sababu damu ni huduma ambayo hainunuliwi mahali popote bali inatoka kwa wananchi kwenye jamii  tunahitaji jamii ijitolee damu kwa hiari lakini muamko wa jamii katika zoezi hili ni mdogo" alisisitiza.

Taasisi ya dini ya kiislamu ya Bilal Muslim Mission Tanzania tawi la Tanga inaungana na hospitali hiyo kuchangia damu hospitalini hapo ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa huduma hiyo. 

Sheikh Sajjad Hassan amesema kuwa uchangiaji wa damu katika hospitali hiyo kawaida yao ya  kila mwaka ikiwa ni ishara ya kuonesha moyo wa kujitolea  wahitaji mbalimbali hususani watoto na mama wajawazito waliopo hospital wanaohitaji kuongezewa damu.



"Lengo la kuja kuchangia damu hapa hospital ni kujitolea sadaka,  tunaifungamanisha sadaka yetu na tukio la kuwawa kwa mjukuu wa bwana mtume (S.A .W) Hussein Bin Ally aliyeuwawa mwaka 61 Hijiria huko Iraq aliyekuwa wakiipigania dini kwa lengo la kukemea mabaya na kuamrisha mema,  aliyetoka kutetea wanyonge  na wale waliodhurumiwa" 

"Na sisi taasisi ya Al Bilal Muslim hili ni zoezi ambalo  tunalifanya kila mwaka tukija kuchangia damu katika maeneo tofauti tofauti lengo na sisi ni kuonyesha kwamba tumesimama pamoja na mjukuu wa bwana mtume (S.A.W) katika kutetea wanyonge,  damu itasaidia wanyonge,  pia tunasimama na kukemea dhuruma zozote  zinazoendelea ulimwenguni" alisema Sheikh Hassan.


INSERT…. SHEIKH SAJJAD HASSAN
Kiongozi shule ya wasichana Zahra centre. 

2.Ustadhat Shekhat Othman
Mwalimu wa Madrasa Bilal Muslim.

Taasisi ya Bilal Muslim imefikia hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kuuwawa kwa mjukuu wa Mtume Imamu Hussein aliyeuwawa katika ardhi ya Karbala Iraq wakati akitetea ubinadamu.

Wanafunzi , walimu pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu zaidi ya 130 kutoka Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania tawi la Tanga wameshiriki kikamilifu katika zoezi la uchangiaji wa damu salama katika hospotal ya rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo ikiwa ni maadhimisho ya mwaka mpya wa kiislamu ukiambatana na kukumbuka kifo cha mjukuu wa Mtume (S.A.W) Imamu Hussein Ally. 
 

Hospitali y rufaa Mkoa wa Tanga ina uhaba wa chupa 200 za damu Hospitali y rufaa Mkoa wa Tanga ina uhaba wa chupa 200 za damu Reviewed by Fahadi Msuya on July 28, 2023 Rating: 5