Header AD

header ads

TUCTA YAWATULIZA WAFANYAKAZI ,NI KUHUSU VIWANGO VIPYA VYA MISHAHARA.




CHAMA cha Wafanyakazi nchini(TUCTA)kimewataka wafanyakazi nchini kuwa na subira wakati serikali ikilekebisha changamoto iliyopelekea kutoanza kulipwa nyongeza ya mshahara uliotangazwa na serikali ambao ilitarajiwa kuanza kulipwa mwezi wa saba mwaka huu.



Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam,Rais wa TUCTA,Tumain Peter Nyamhokya ametaja sababu iliyopelekea ni kuwa ya kitaalamu.

"Tumeongea Serikali na serikali imeahidi kukamilisha suala hili kupitia mishahara itakayotolewa kwa wafanyakazi mwezi Agosti mwaka huu"Amesema Nyamhokya.

Hata hivyo,Nyamhokya  ameiomba serikali kutekeleza suala hilo muhimu kama ambavyo imeahidi ili kuendelea kuongeza morali kwa wafanyakazi katika kufanyakazi na kutoa huduma..

Nyongeza hiyo ya mshahara ni ile iliyohaidiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais Samia Suluhu Hassan,kwenye sherehe za mei mosi mwaka huu ambapo ilitangaza kwaanzia mwaka mpya wa fedha   2023/2024 kwa wafanyakazi ni pamoja na nyongeza ya mshahara ya kila mwaka katika mishahara ya wafanyakazi kwa kuzingatia miundo ya mishahara kwa kila kada na kidato.
TUCTA YAWATULIZA WAFANYAKAZI ,NI KUHUSU VIWANGO VIPYA VYA MISHAHARA. TUCTA YAWATULIZA WAFANYAKAZI ,NI KUHUSU VIWANGO VIPYA VYA MISHAHARA. Reviewed by Fahadi Msuya on July 26, 2023 Rating: 5