Header AD

header ads

RC KINDAMBA AWATAKA WATANZANIA KUCHUKUA TAHADHARI



Na Hadija Bagasha Tanga, 

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amewataka watanzania kuchukua tahadhari na wale wote wanaohubiria watu kubaguana ikiwa ni pamoja na wenye nia mbaya ya kuvuruga umoja, mshikamano na amani ya nchi iliyopo ambao wana nia ya kuwatenganisha watanzania. 

Mkuu wa Mkoa ametoa kauli hiyo wakati akifungua  kikao cha warsha ya uelimishaji wa umma  kuhusu maandalizi ya Dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2050 kilichoketi Mkoani Tanga. 


Kindamba amesema kuwa zoezi hilo linalenga kwenye kutoa elimu kwa viongozi na wawakilishi wa makundi mbalimbali kuhusu dira lakini pia zoezi hilo litasaidia kujenga uelewa kwa viongozi katika Mkoa, wilaya na Halmashauri kuhusu mchakato wa maandalizi ya dira ya maendeleo ya 2050 ambapo amewaasa wananchi kuwapuuza wale wote wenye nio ovu kuhusu zoezi hilo. 

"Nchi yetu imefumwa vizuri na waasisi wa Taifa hili tusiruhusu wachache wenye nia mbaya ya kuvuruga umoja wetu,  mshikamano wetu,  natolea mfano msusi wa ukili wewe unafuma halafu huku mwingine anafumua hamuwezi kujenga Taifa la namna hiyo bali kitakachofuata hapo ni vurugu tu sio nchi,"alisistiza Kindamba. 


Aliongeza kuwa Mataifa makubwa duniani yanafikiria kuungana halafu sisi na mataifa madogo madogo tunafikiria kutengana ujue kuna shida hapo na ni lazima tuchukue hatua na tuwe na tahadhari kubwa yeyote anayehubiri kubaguana miongoni mwetu kwasababu yeyote ile lazima tuwe na tahadhari naye kwasababu anataka kutupeleka mahala pabaya. 

"Mataifa makubwa kabisa yaliyoendelea  duniani huwa yanakuwa na vision kwahiyo chama chochote kitakachoingia madarakani au kilichopo madarakani kitakuwa na Vision kwahiyo nimefurahi kuona vyama vyote viko hapa ili tunapoitengeneza hii dira hapo baadae hata kama nyinyi mtashika madaraka mtembee na dira hiyo hiyo kwasababu inakuwa ni dira iliyojumuisha wote, "alisema Kindamba. 

Aidha Kindamba amesema kuwa wanapokwenda kutengeneza dira ya nchi ni vyema wakawajumuisha wanataaluma mbalimbali wenye uzoefu mbalimbali ili kuweza kufanikisha zoezi hilo ipasavyo. 

Amesema dira ya Taifa ya maendeleo imegusa makundi yote hivyo anatarajia kutakuwa na ushirikishwaji wa wadau wote katika ngazi zote ikiwemo taasisi za elimu juu ya utafiti,  sekta binafsi na asasi za kiraia na wananchi mmoja mmoja ushirikishwaji wa wadau utawezesha kupata dira jumuishi itakayokidhi mahitaji stahiki kwa Taifa katika kipindi cha miaka ijayo. 

Kwa upande wake Mwenyekiti kamati ya uandishi dira ya Taifa ya maendeleo 2050 Gladness Salema amesema kuwa  zoezi hilo ni la kimkakati na ni zoezi ambalo sio suala la kuchagua bali  ni lazima kazi hiyo ifanyike kwa uaminifu na uadilifu



"Tuondoe kabisa tofauti zetu tuondoe kabisa ubinafsi tuangalie kwamba tunahitaji Tanga ambayo watanzania waliopo Tanga wanaitaka nasisitiza pia umuhimu wa kushiriki katika zoezi hili pamoja na kwamba linaitwa Dira ya Taifa mchakato wake umeanzia huku chini kwasababu tuna tofauti ndani ya Taifa hili ukingalia kwenye jamii zetu tuna mila na desturi,  hata katika mazigira gografia zetu tuna tofauti katika kumiliki rasilimali za asili, "alisema Salema. 

Sosthenes Kewe Mwezeshaji timu ya  dira 2050 amesema kwa ujumla utekelezaji wa dira 2025 umechochea kasi ya ukuaji wa uchumi kwa wastani wa zaidi ya asilimia 6 kwa mwaka katika kipindi chote cha utekelezaji wa dira. 

Nguzo za dira 2025 zipo tano ikiwemo kuboresha hali ya maisha ya watanzania, kujenga uchumi imara na shindani,  kuwepo kwa mazingira ya amani,  usalama na umoja,  kujenga utawala bora,  kuwepo jamii iliyoelimika vyema na inayojifunza. 


RC KINDAMBA AWATAKA WATANZANIA KUCHUKUA TAHADHARI RC KINDAMBA AWATAKA WATANZANIA KUCHUKUA TAHADHARI Reviewed by Fahadi Msuya on July 26, 2023 Rating: 5