Header AD

header ads

WAKURUGENZI WA WAKUU WANUNUZI WA DAWA SADC WAVUTIWA NA MSD,





WAKURUGENZI Wakuu,Watendaji wakuu pamoja na wakuu wa manunuzi wa Taasisi zinazosimamia ununuzi bidhaa za afya kutoka nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SDC) wamekutana nchini Tanzania kwa lengo la kujadili masuala yanayohusu uboreshaji wa manunuzi ya bidhaa za afya katika mfumo wa SADC.

Akizunguza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) nchini Mavere Tukai amesema wakuu hao wamekutana kwa lengo la kuweka mkakati wa ununuzi wa pamoja wa SADC ambao umeanza mwaka 2019 na MSD ndio iliyopewa jukumu la kununua na bado inaendelea.

“Kutokana na changamoto kama vile za COVID-19 pamoja na changamoto nyingine mbalimbali huu uliyumba katikati hapa kwa hiyo Sekretarieti ya SADC na MSD tushirikiane kupitia kuangalia kwanini hatuvuki malengo au hatufiki ambako tumepanga.Pamoja na COVID je kuna kitu gani tunaweza kufanya tukaboresha zaidi , mambo gani tumejifunza SADC kwa muda ambao tumekuwa tukitoa huduma kwa miaka kadhaa.

“Kwa hiyo tulikuwa tumekutana baada ya kazi kubwa iliyokuwa imefanyika na Sekretariet ya SADC na MSD kwa kupata msaada wa Umoja wa Ulaya kuangalia tunafanyaje kuboresha mfumo wa manununuzi wa SADC.Kikao hiki ambacho tumekutana ni kujakupokea taarifa ya mapitio tuliyoyafanya kuangalia maboresho, lakini tunaiwaje MSD kuendelea kuwa mdau mkuu katika ushiriki wote na kwa kuwa bado iko hapa nini kinatakiwa kufanyika kuboresha.

“Sasa timu ile ya wataalam bingwa kushirikiana na sisi tulifanya mapitio, yalikuwepo mapendekezo kadhaa ya muda mfupi, kati na muda mrefu na lengo ni kuhakikisha mfumo huo wa manunuzi kwa nchi za SADC unafanya kazi vizuri , kwa hiyo palikuwa na uwasilishaji wa kilichoonekana kama maeneo ambayo yanafanya vizuri na kwenye changamoto,”amesema Tukai

Hivyo amesema wamekutana kuangalia mapendekezo ya nini kifanyike ili mfumo ufanye vizuri kwani kama inavyofahamika ni mfumo wa manunuzi wa SADC na sio kwamba ni mfumo wa MSD, ni nchi 16 zote zinashirikiana kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya kwa pamoja na wao wamekabidhiwa jukumu hilo kuendesha huo mfumo wa manunuzi kwa nchi hizo

Aidha amesema kabla ya utekelezaji kuna hatua mbalimbali zinafikiwa kwasababu hilo jambo ni la kimataifa sio la Tanzania peke yake , kwa hiyo mapendekezo yote ya timu ya watalaam , wamekuwa na viongozi wa bohari za dawa kutoka nchi 16 na wafamasia wakuu pamoja na viongozi wa Wizara na walichopendekeza wapokee kwenye baraza la SADC makao makuu watakaa kutengeneza taarifa yao kama timu ya watalaam .
WAKURUGENZI WA WAKUU WANUNUZI WA DAWA SADC WAVUTIWA NA MSD, WAKURUGENZI WA WAKUU WANUNUZI WA DAWA SADC WAVUTIWA NA MSD, Reviewed by Fahadi Msuya on July 14, 2023 Rating: 5