WANAHARAKATI WA MAJI WAIANGUKIA SERIKALI,WATOA YAMOYONI.
KATIKA kuhakikisha wanapambana na uhalibifu wa Mazingira,Wanaharakati wa Maji Mkoa wa Dar es salaam wameiomba serikali kuingilia kati uharibifu mito unaofanywa na baadhi ya viwanda vinavyodaiwa kutitirisha maji ya kemikali katika mito hiyo.
Wanaharakati hao pamoja na wakazi wa mtaa wa mabibo farasi Kata ya Mabibo Wilaya ya Kinondoni katika Mkoa huo wamepaza sauti zao wakati wakizungumza na vyombo vya habari ambapo wamedai kuwa maji hayo yamekuwa yakisababisha kero kwa wakazi hao.
Wamesema kuwa kuwa wananchi wa hali ya chini ndio wanaoathirika na maji ya mto huo kutokana na kutumia mbombamboga zinazonyeshelewa na maji hayo lakini pia na shughuli mbalimbali wanazozifanya katika mto huo.
"Mto huu unatumiwa na watu wengi sana hasa wa Hali ya chini kwani kitendo wanachokifanya kinapelekea kuleta madhara kwa wananchi"wamesema Wanaharakati hao
Miraji Awadi Simba ni Katibu msaidizi wa wanaharakati wa maji na mazingira Mkoa wa Dar es salaam amesema huo umekuwa ni mwendelezo wa kupaza sauti kuibua kero zilizopo katika mito mbalimbali katika mkoa huo.
"Tunaomba Kwa sauti hii Mhe Dkt Samia Suluhu uweze kutusaidia wabadilishe miundombinu ya huu mto chemba Yao waangalie pa kuweka kwani tunatamani Viwanda vyote vya Mkoa wa Dar es salaam viweze kufungwa Ili warekebishe Miundombinu ya Viwanda vyao"amesema Miraji
Kwa upande wake Mjumbe na Mwenyekiti wa kamati ya Mazingira wa Mtaa wa mtaa wa mabibo farasi Kata ya Mabibo Mashaka Sabani amekiri changamoto zinazotokana na kiwanda hicho na kudai wameshawahi kuzifuatilia lakini hakuna ufumbuzi.
WANAHARAKATI WA MAJI WAIANGUKIA SERIKALI,WATOA YAMOYONI.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
July 31, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
July 31, 2023
Rating:

Post a Comment