Header AD

header ads

WENGI WAVUTIWA NA UTALII WA PICHA, BOTI HIFADHI YA TAIFA NYERERE.




Na. Sixmund Begashe

Hifadhi ya Taifa Nyerere iliyopo Mkoani Morogoro, imekuwa kivutio cha wa Watalii wengi kutoka ndani na nje ya nchi, kwa Utalii wa Boti na Upigaji picha wa vivutio mbalimbali vilivyopo majini na pembezoni mwa Mto Tufiji.

Akizungumzia sababu ya wengi kuvutiwa na Utalii, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Nyerere, Ephrahim Mwangomo amesema viivutio lukuki vilivyopo, miundombinu rafiki na ukubwa wa Hifadhi unatoa fursa kwa Watalii ya kutokusanyika eneo Moja kuona vivutio.


Kamisheni Msaidizi Mwangoma ameongeza kuwa, kupitia Mradi wa Kukuza na Kuendeleza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW), Hifadhi imepata Magari, Vifaa mbalimbali kwaajili ya Uhifadhi, Mitambo ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu, ili kuimarisha mvuto wa Hifadhi Kwa Wageni  wanapotembele.

Akizungumzia uzoefu alioupata katika Hifadhi hiyo, Mtalii Wendy kutoka Marekani, amesema ni zaidi ya matarajio yake na watoto wake Kuona vivutio vingi ndani ya mazingira yanayovutia sana na kuwa Balozi mzuri wa kuwashawishi ndugu na marafiki zake kutembelea Hifadhi ya Taifa Nyerere.


WENGI WAVUTIWA NA UTALII WA PICHA, BOTI HIFADHI YA TAIFA NYERERE. WENGI WAVUTIWA NA UTALII WA PICHA, BOTI HIFADHI YA TAIFA NYERERE. Reviewed by Fahadi Msuya on July 20, 2023 Rating: 5