Header AD

header ads

CCM TANGA YATOA MAELEKEZO WILANI KOROGWE



Na Hadija Bagasha Korogwe, 

Chama cha mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Tanga kimesema hakikuridhirishwa na kasi ya ujenzi wa vituo vya afya katika kata ya Mnyuzi na Kerenge vilivyopo Wilayani Korogwe Mkoani Tanga  ambavyo serikali imeleta fedha kwajili ya vituo hivyo ambavyo hadi sasa havijakamilika. 

Kufuatia hatua hiyo chama cha mapinduzi ccm Mkoa Tanga kimemuagiza Mkuu wa wilaya ya  Korogwe Jokate Mwegelo kufuatilia kwa karibu miradi ya vituo hivyo ili kuhakikisha vinakamilika kwa wakati na kutoa huduma stahiki kwa wananchi. 


Akizungumza wakati wa ziara yake wilayani humo ya kuona uhai wa chama na kukagua shughuli za kimaendeleo,  Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga Rajab Abrahaman Abdallah akatoa maagizo baada ya kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa vituo hivyo ambavyo serikali imeleta fedha kwajili ya vituo hivyo ambayo hadi sasa havijakamilika. 

Akitoa Maelezo kuhusiana na Ujenzi Wa Kituo Cha afya kilichopo kijiji cha Mkwakwani kata ya Mnyuzi Mganga Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Dkt Mariam Cheche alisema awamu ya kwanza walipokea shilingi milioni 250 kwajili ya kujenga jengo la wagonjwa wa nje (OPD), maabara na kichomea taka fedha ambazo zilitumika bila kukamilika kwa majengo hayo. 


Alisema serikali ilileta tena shilingi milioni 250 kwa ajili ya kujenga jengo la mama na mtoto, jengo la kufulia na njia tembezi.

"2020/21 serikali ilitoa kiasi cha shilingi milioni 250 kwajili ya ujenzi wa kituo cha afya Mnyuzi ambapo kilikuwa kinatakiwa kijengwe majengo ya OPD,  Maabara na. Kichomea taka lakini mwaka 2022/23 serikali ilileta tena shilingi milioni 250 kwajili ya kuendelea na ujenzi ambao mpaka sasa jengo letu la mama na mtoto linaendelea na kazi mbalimbali, huku kichomea taka kikiwa hakijajengwa na fedha haikutosha "alisema Mganga mkuu huyo. 

Alipoulizwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini khalfan Magani alisema mradi huo umeshindwa kukamilika kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mkandarasi kuchelewesha ujenzi huo licha ya kulipwa fedha.

"Fedha iliyoliwa hapa ni shilingi milioni 110, huku ndiyo kumsaidia mheshimiwa Rais, huko ndiyo kukisaidia Chama Cha Mapinduzi hivi mko serious kwelii?" alihoji Mwenyekiti Rajab. 

Mwenyekiti Rajab alisema kwamba Korogwe wana mkuu wa wilaya makini, lakini wameshindwa kusimamia miradi hiyo ili iweze kumalizika kama kusudio la serikali kujenga vituo vya afya kusogeza huduma karibu na wananchi badala ya kutembea umbali mrefu.

Alisema serikali imetoa fedha nyingi ili kuondoa kero kwa wananchi na kwamba ili fedha ziweze kuletwa kwa ajili ya miradi ya Maendeleo wabunge katika maeneo ya wananchi wamepiga kelele lakinj usimamizi wa fedha hizo umekuwa mdogo kwa watendaji.


"DC wenu ni mtu makini sana, sasa naomba nitoe maelezo hapa, mkuu wa wilaya fuatilia miradi hii ya vituo vya afya hadi mradi ukamilike lakini pia vyombo vyako vifanyr ukaguzi wa matumizi ya fedha wale watakaobainika wamechezea fedha za serikali chukueni hatua za kisheria," alisema.

Sambamba na hayo Mkurugenzi alisema kuhusu vituo hivyo vya afya tayari kuna watumishi wa halmashauri hiyo wamechukuliwa hatua za kisheria kutokana na madai ya kutumia fedha vibaya za miradi hiyo.


CCM TANGA YATOA MAELEKEZO WILANI KOROGWE CCM TANGA YATOA MAELEKEZO WILANI KOROGWE Reviewed by Fahadi Msuya on August 07, 2023 Rating: 5