DC Temeke awapongeza ladies of new millennium kusaidia watoto wakike
Na Iddy Ally
MKUU wa Wilaya ya Temeke Mheshimiwa Mobhare Matinyi amewapongeza Ladies Of New Millennium kwa kuunga mkono Juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Sekta ya Elimu inaendelea kuwa msaada mkubwa kwa vijana, watoto kwani wao ni hazina ya jamii.
Kiukweli nawashukuru Sana wakinamama wa Ladies Of New Millennium kwa kuamua kuja Leo hapa wilaya ya Temeke maana sote tunajua Rais Samia ana mambo mengi ya kufanya na hivyo wao kutenga muda kuja ni Jambo zuri.
Aidha, Mkuu Wa Wilaya ya Temeke Mheshimiwa Mobhare Matinyi amewashukuru walimu wanaoendelea kulea watoto hao mashuleni, Raisi wetu amehakikisha watoto wanapata Elimu bure lakini anaendelea kutoa hela nyingi Kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ,hii yote ni ili kuboresha kesho ya watoto.
"Mtoto ni hazina ya jamii na tunategemea wawe viongozi wa baadae Nchini hivyo wote tuungane ili kuimarisha ulinzi wa watoto , watoto walindwe kama mboni ya jicho, Hedhi ina changamoto zake ambazo kama zisipotatuliwa basi zinaweza pelekea watoto kushindwa kuhudhuria shule vyema , Leo tunagawa pedi Kwa watoto hawa na kama mmeona tumetengeneza dispenser nzuri za pedi pale shule ya Mtoni " Mama Mary Majaliwa.
"Nimeingia ndani na kuona maboresho , jengo ni zuri na Pia upatikanaji wa taulo sasa ni wa uhakika hapa shule ya msingi Mtoni, Watoto wetu wataendelea kujihifadhi vyema na kuhudhuria vipindi ,tusisikie tena mtoto amerudi nyumbani Kwa sababu ya Hedhi labda tu ugonjwa." ~ Mama Mary Majaliwa .
Mama Tunu Pinda amesema leo tumekutana na wanafunzi ambao ni watoto wazuri,wachangamfu, niwashukuru wanawake Kwa hili la kujenga eneo la kujisitiri watoto wa kike shule ya msingi Mtoni, Mradi huu wa kuboresha Vyoo na kuweka sehemu ya kujisitiri ni mwanzo na utakua endelevu mpaka tutakapomaliza shule zote Nchini na tumeungana na Wizara ya Afya na Maendeleo ili kuweka dawati la jinsia Kwa kila shule
"Umri wa watoto kuanzia miaka 5 hadi 15 ni Asilimia 42% ya Watu wote Tanzania ndio maana kina mama wameona umuhimu wa kusaidia kupambana na madhara yanayoambatana na Ukuaji wa Teknolojia, Watoto wa Leo ndio viongozi wa kesho , Sisi tuna lengo la kua na Taifa Bora kesho ndio maana tunaona hata Elimu ni bila malipo , tusikubali kuiga kutoka nje ,tupate Elimu ya hapa ndani". Mwantumu Muhiza Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali
"Kwa niaba ya HQ Tanzania tumeweza kuchangia jumla ya boksi 300 za pedi na Lengo ni kumuimarisha mtoto wa kike ili aje awe mbunge ajae hata ikiwezekana Rais, Nitashirikiana na Millennium foundation kwenye kila shule ambayo wataenda kukarabati na kutengeneza hizi dispenser maana nimeona Lengo Lao ni zuri Sana " Selina Letara Mkurugenzi Human Cherish Pads
"Kwa kuanza tumebuni mradi wa kusaidia watoto wa kike wakiwa kwenye Hedhi ili waweze kujisitiri. Ni mradi tutakaoufanya kwenye shule zote za Serikali za nchi yetu pendwa, Sisi tunakarabati vyoo na kuhakikisha tunaweka mahitaji yote ya mtoto wa kike anapokua kwenye Hedhi kwani tunaamini mtoto wa kike anapaswa kuhudhuria masomo siku zote". Arafa Kikwete Katibu wa Ladies of New Millenium
DC Temeke awapongeza ladies of new millennium kusaidia watoto wakike
Reviewed by Fahadi Msuya
on
August 07, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
August 07, 2023
Rating:




Post a Comment