Header AD

header ads

MAKAMPUNI 500 KUTOKA ASIA NA INDIA KUTUA NCHINI.





JUMLA ya Makampuni 500 toka India na Asia wanatarajia kushiriki  mkutano wa kimataifa wa Chakula ambao kwa mara ya kwanza unafanyika Barani Afrika nchini Tanzania katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam Agosti 10 hadi 12.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TASO Event Suveer Rajpuexlint amesema kupitia mkutano huo utajenga ushirikiano kati ya India na nchi za Afrika kwenye maswali ya kiuchumi kibiashara na kijamii.

Aidha amesema mahusiano kati ya Afrika na India yanazidi kukua hususani sekta ya kilimo kwani changamoto za wakulima Afrika zinafanana na za India hivyo lengo lao ni kukuza wakulima wadogo na kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na India kwenye bidhaa za kilimo.


Aidha amesema kwa kushirikiana wataweza kukabiliana na changamoto zilizopo na kuimarisha zaidi mahusiano yao na kuongeza uwekezaji kutoka India ambao utaongeza pato la taifa kwani India ni soko kubwa kwa nchi za Afrika hivyo Afrika wanakaribishwa kuwekeza nchini humo.

Amesema teknolojia pia inasaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo zile za mabadiliko ya hali ya hewa, na uhaba wa maji hivyo wakishirikuana kwa pamoja na kutatua changamoto wataweza kuzalisha bidhaa na kuilisha Afrika na Asia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Tanzania Pulses Network (TPN) Lirack Andrew amesema dhima ya mkutano huo ni kufungua masoko kwa mazao ya Afrika na kutoa taarifa kwa duniani nzima kuhusu uzalishaji uliopo Afrika ili nchi zenye uhitaji zifahamu na kuagiza bidhaa kutoka Afrika.
Aidha amesema kupitia maonyesho yatakayofanyika wanatarajia kupokea watu zaidi ya 3000 ambao watatembelea mabanda ya wafanyabiashara na makampuni hivyo kujifunza mambo mbalimbali na kubadilishana uzoefu.
Sambamba na hayo ametoa wito kwa wananchi kushiriki kwa wingi katika maonyesho hayo ambayo yatawawezesha kujenga mahusiano na kampuni za nje zitakazoshiriki kwenye maonyesho hayo na kukuza teknolojia zao na kupata fursa za masoko ya bidhaa zao.
MAKAMPUNI 500 KUTOKA ASIA NA INDIA KUTUA NCHINI. MAKAMPUNI 500 KUTOKA ASIA NA INDIA KUTUA NCHINI. Reviewed by Fahadi Msuya on August 09, 2023 Rating: 5