WAZIRI MKUMBO AMTAJA RAIS SAMIA KWENYE UWEKEZAJI,AFANYA ZIARA KWENYE VIWANDA HIVI.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo,amesema uwepo sera nzuri,usalama wa nchi na uongozi safi wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassani ni jambo linalowavutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini na kusaidia kuongeza ajira na kukuza uchumi.
Profesa Mkumbo ameyasema hayo leo wilaya ya mkulanga mkoa wa Pwani wakati alipokuwa anafanya ziara ya kukagua uwekezaji ambapo ametembelea kiwanda
cha Knauf Gypsum Tanzania Limited ambapo kinatengeneza Gypsum pamoja na kiwanda cha Sapphire floot glass.
"Sera nzuri ya uwekezaji ya Rais Samia ndio imewafanya wawekezaji wakubwa kama hawa kuja kujenga kiwanda hapa,na agenda yake ya Rais ya kuvutia mitaji,ajira imetimia kutokana uwekezaji huu"amesema
Aidha,Profesa Mkumbo amesema lengo la wizara yake kuweka mazingira mazuri ya wawekezaji kuja nchini ,pili kuhakikisha wanawekeza pamoja na uwekezaji unafanyika.
Akizungumzia ujenzi kiwanda cha Sapphire floot glass ,Profesa Mkumbo,amesema kiwanda hicho kimeanza ujenzi wake julai 202 na kitarajia kuanza uzalishaji mwezi sempemba mwaka huu.
"Kiwanda hiki ni cha nne kwa ukubwa Afrika,kinatarajia kuzalisha ajira kwa watanzania elfu saba,kitawezesha kuuza bidhaa nje ya nchi na kuongeza mapato yote inatokana na sera nzuri ya Rais Samia"Ameongeza kusema.
Mbali na kiwanda hicho,Profesa Mkumbo,amekizungumzia kiwanda cha Knauf Gypsum Tanzania Limited ambapo uwekezaji wake umetumia zaidi ya Bilioni 250 na kinatoa ajira za moja kwa moja 140 na wanarajia kupanua kiwanda kile na kuwa mara tatu.
"Mmeona uwekezaji mkubwa kama huu kwahiyo watu wanaosema uwekezaji hajafanyika nchini wajue,na lengo langu kutimiza agenda ya Rais Samia"Amesema Waziri Mkumbo.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini(TIC),Gilead Teri,amesema kwa sasa nchini kuna mazingira mazuri ya uwekezaji na kwa sasa kituo hicho kimejipambanua katika hilo.
"Kwa sasa serikali imewaondolea asilimia 75 ya kodi kwa wawekezaji wanapoagiza vitu jambo lilowavutia"
" sisi TIC tumeunda kanda kwa ajili kutembelea wawekezaji ili kuwasikiliza na kuangalia changamoto wanazokutana nazo"Amesema Teri.
WAZIRI MKUMBO AMTAJA RAIS SAMIA KWENYE UWEKEZAJI,AFANYA ZIARA KWENYE VIWANDA HIVI.
Reviewed by Fahadi Msuya
on
August 09, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
August 09, 2023
Rating:

Post a Comment