IJA kutoa mafunzo kwa ufadhili wa benki ya Dunia
Chuo cha uongozi wa mahakama (IJA) Lushoto kinatarajia kuingia kwenye mfumo wa kiteknolojia wa kutoa mafunzo kwa ufadhili wa benki ya dunia na kwa zaidi ya miezi mitatu wataalamu wanaendelea kuujenga mfumo huo.
Jaji Paul Kihwelo ambaye ni Mkuu wa chuo cha uongozi wa mahakama (IJA) Lushoto amesema kuwa mfumo huo wa kutoa mafunzo kwa njia ya kiteknolijia unajengwa kwenye katika chuo hicho kwasababu ndio chenye dhamana ya kutoa mafunzo na utafiti.
"Kwa sasa tunapozungumza kwa zaidi ya miezi mitatu wataalamu wapo chuoni wanaujenga mfumo huo wa kutoa mafunzo kwa njia ya teknolojia na mfumo huo hatua za awali zimeshaanza kukamilika na utawawezesha mahakimu na majaji kujifunza kupitia teknolijia hiyo, "alisisitiza Jaji Kihwelo.
Wakizungumza kwenye kikao cha baraza la wafanyakazi wa chuo hicho ,baadhi ya washiriki wamesema mfumo huo utaongeza kiwango cha wanafunzi watakaosoma masomo ya sharia kwa jia ya masafa tofauti na mfumo wa kukaa darasani unaotumika kwa sasa.
Patricia Kisinda ambaye ni Mjumbe wa baraza amesema kuwa chuo hicho kwa kushirikiana na mahakama Tanzania wameweza kutengeneza mfumo huo utakaowawezesha kuwajengea uwezo maafisa wa kimahakama majaji na mahakimu katika shughuli zao za kimahakama.
"Ni sehemu pia ya sisi kujifunza na kwasababu umuhimu wa mafunzo haya ni mkubwa sana kwenye taasisi kwa kuwa baraza la wafanyakazi ni mkusanyiko wa watu wanaowakilisha maslahi ya marneo mbalimbali katika taasisi, "alisema Katarina Mteule-Jaji Mfawidhi Mahakama kuu kanda ya Tanga.
Mfumo huo ambao unafadhiliwa na benki ya dunia unatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2024 na kuanza kutoa huduma kwa jamii ikiwa ni mpango wa maboresho wa huduma za kimahakama hapa nchini .
IJA kutoa mafunzo kwa ufadhili wa benki ya Dunia
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 11, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 11, 2023
Rating:

Post a Comment