TEA INAJIVUNIA WANUFAIKA ZAIDI YA 49,000 WA MAFUNZO YA UJUZI (SDF)
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) inajivunia kuwa na wanufaika zaidi ya 49,000 nchi nzima walionufaika na mafunzo ya kuongeza ujuzi yaliyoendeshwa na vyuo mbalimbali chini ya Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) unaoratibiwa na mamlaka hiyo.
Akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima ambalo maonesho yake kitaifa yanafanyika Wilayani Kibaha mkoani Pwani, afisa habari wa Mradi wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) Bi. Eliafile Solla amesema kuwa wengi wa wanufaika hao kwa sasa wamejiajiri na waliosalia wameajiriwa kutokana na mafunzo waliyoyapata.
“Kwa wale waliojiajiri wameendelea kukuza wigo wa ajira kwa kuendelea kuajiri watu wengine kwenye shughuli zao za kibiashara”
Mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi yanayotolewa na vyuo mbalimbali vyenye ithibati kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yamejikita kwenye sekta sita za kipaumbele ambazo ni kilimo na kilimo uchumi, uchukuzi, ujenzi, teknolojia ya habari na mawasiliano, utalii na huduma za ukarimu pamoja na nishati
Maadhimisho ya “Juma la Elimu ya Watu Wazima” linatarajiwa kufikia tamati Ijumaa, Oktoba 13 mwaka huu huku idadi ya watu wazima wanaojua kusoma na kuandika ikitajwa kuongezeka.
TEA INAJIVUNIA WANUFAIKA ZAIDI YA 49,000 WA MAFUNZO YA UJUZI (SDF)
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 12, 2023
Rating:
Reviewed by Fahadi Msuya
on
October 12, 2023
Rating:


Post a Comment